08/04/2022
*SUPER GRO*
Super Gro ni Kirutubisho bora asilia cha Mimea kisicho na kemikali ambacho kilitengenezwa ili kuhakikisha uimarishaji wa mazao yako katika hali ya majira yoyote pia huongeza uzalishaji wa mazao kwa ubora wa hali ya juu kwa kilimo chochote. Kirutubisho hichi asilia chenye sifa kutoka kwa wakulima wote duniani ambacho kitaongeza mazao yako zaidi ya mara tatu unayoweza kupata kutoka kwa mbolea zingine za kemikali.
Super Gro ni bidhaa ya NEOLIFE, Hii ni kampuni ambayo kitaalamu inatengeneza na kusambaza duniani kote bidhaa za asili na lishe kwa binadamu na mimea .Super Gro ni kirutubisho cha maji kwa mimea ambacho hakina kemikali kabisa iliyoongezwa au kuchanganywa nayo,hiki kirutubisho ni salama kwa asilimia 100% kutumia kwenye mboga au mazao yoyote. Super Gro inaweza kutumika kwa mimea yoyote, mti, mboga na majani ambayo yanahitaji mbolea.
_HISTORIA_
Super Gro ilianzishwa karibu miaka 15 iliyopita kwenye Pwani ya Magharibi ya Afrika Kusini. Kiungo chake kikubwa kuwa ni mbolea ya seabird(aina ya ndege) hupata kukusanywa kutoka maeneo tofauti nane kando ya Pwani ya Magharibi chini ya usimamizi wa Uhifadhi wa Hali ya Afrika Kusini, ili kuhakikisha kwamba ndege hao wote wanaish kwenye mazingira mazuri bila uharibifu wa mazingira hayo wanayoishi.
Uzuri wa Super Gro ni kwamba haina kemikali au chembechembe inayo adhiri usalama wa afya ya binadamu kwa sababu haina mabaki ya kemikali ambayo yanaweza kubaki katika mazao ya kilimo ambayo inaweza kuweka maisha ya binadamu katika hatari katika mchakato wa matumizi . Hivyo basi,kutokua na kemikali hii mbolea ni rafiki kwa udongo wowote bila kuleta madhara.
*KAZI ZA SUPER GRO*
1>Kusaidia udongo kutunza unyevunyevu kwa muda mrefu(wetting agent) kwani Super Gro huvunjavunja uzio wa maji na kuruhusu kupenya hadi tabaka la 3 la udongo
2>Kuongeza uzalishaji kwa maana ya wingi na ubora wa mazao.
3>Husaidia mimea kufyonza virutubisho vilivyomo katika udongo hasa katika tabaka la 3 la udongo kwani hufanya mizizi ya mimea kupenya ktk tabaka hilo na kufyoza virutubisho vyote muhimu hivyo mimea kuwa imara na yenye afya
4> Kusaidia dawa za kuulia wadudu zisitiririke (Sticker)na zifanye kazi ipasavyo, hivyo kupunguza garama za dawa na pembejeo zingine za kilimo
5>Kupunguza garama za mbolea(hadi kufikia nusu) kwani kwa kutumia Super Gro utatakiwa kutumia kiac kidogo sana cha mbolea
6>Kufanya mimea iwe na rangi halisi ya ukijani kwani ukijani huo ndio unasaidia mmea kujitengenezea chakula chake