20/06/2024
• Nilipokea maoni ya wadau tofauti, baada ya kuandika makala ndefu yenye maelezo ya kina kuhusu unafuu wa bidhaa za electronics pamoja na gharama za usafiri kutoka Zanzibar kwenda Tanzania Bara.
• Wengi walionesha kuvutiwa kwa unafuu wa bei uliopo, baadhi yao walinitafuta ili kupata majibu ya maswali wanayo jiuliza!
• Binafsi nilibaini mambo kadhaa, ikiwemo wengi wao kukabiliwa na hofu ya kupoteza. Ni dhahiri inaonesha kwamba bado swala la udanganyifu mitandaoni limebaki kuwa ni kikwazo!
KUPITIA POST HII
Nataka uwafahamu matapeli wanaotumia njia hii kukulangai!👇
▫️Hujivisha vinyago vyenye haiba ya Zanzibar ili kuficha dhamira zao mbaya.
▫️Mbinu yao ya kujifanya wapo Zanzibar, kwa ku-deal na uuzaji wa ELECTRONICS bila shaka inawapa matokeo mazuri!
▫️Hutumia mitandao kuonesha bidhaa ambazo ki-uhalisia hawana!
▫️Huweka bei za kuvutia ili kuwanasa wale wasio na uelewa!
▫️Hupenda kutumia location ya PEMBA, ambapo kiuhalisia Pemba sio chimbo la vifaa vya electronics!
▫️Ni rahisi kukufanyia punguzo kwa asilimia kubwa ilimradi uingie kingi!
▫️Ukiwapigia simu watakwambia "tuma pesa nusu ili tukutumie mzigo, nyengine utamalizia ukipokea mzigo wako"
▫️Yani ukiwa na pupa na tamaa, ni rahisi sana kunasa kwenye mtego. Mana bei zao zinashawishi kwelikweli!
• Kwa kweli inasikitisha sana kuona watu wengi wananasa kwenye mitego hiyo!
• Hayo yanatokea, kutokana na Matapeli hao kujivisha kinyago cha Uzanzibari, jambo ambalo ni kinyume na uhalisia wao!
• Unafuu wa bei pamoja na sifa ya Uaminifu kwa Wazanzibari, ndio sababu ya matapeli wengi kujivisha kinyago hicho!
• Ukweli ni kwamba, wengi wanaotumia mbinu hizo ili kulaghai, kiuhalisia huwa hawapo Zanzibar!
Binafsi nimefanya tafiti za kutosha kuthibitisha hilo!
Mfano:👇
Instagram:
Na zanzibar_electronics_og
• Hizo ni account mbili tofauti za Instagram, Wanajifanya wapo zanzibar, na ukiangalia accounts zao kwa kiasi fulani zinashawishi, ila kwa 100% ni MATAPELI.
• Watu k**a hawa ndio wanao haribu haiba ya Zanzibar, na kupelekea mambo kuwa magumu kibiashara!
🔸Epuka pupa na tamaa, hawa jamaa ni wabaya sana kwa kucheza na akili za watu! | KUWA MAKINI.
✍️