JE WAJUA.

JE WAJUA. Your wellcome

JE WAJUA KUWA KOREA KASKAZINI KUNA SHERIA INAYORUHUSU MITINDO 28 TU YA NYWELE?Inawezekana kabisa ukawa hufahamu hili,lak...
07/06/2022

JE WAJUA KUWA KOREA KASKAZINI KUNA SHERIA INAYORUHUSU MITINDO 28 TU YA NYWELE?

Inawezekana kabisa ukawa hufahamu hili,lakini ndiyo ilivyo.

Nchi ya Korea Kaskazini ambayo jina lake rasmi ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK) ina sheria maalumu iliyothibitishwa na serikali ambayo inayoelekeza aina ya mitindo ya nywele kwa wanawake na wanaume wa nchi hiyo ya Kijamaa.

Jarida la Time la Marekani liliwahi kunukuu gazeti la Telegraph mwaka 2013 kuwa katika nchi ya Korea Kaskazini wanawake wameruhusiwa kuchagua mitindo 14 iliyoidhinishwa na serikali ya nchi hiyo ambapo wanawake walioolewa wameelekezwa kuwa na nywele fupi huku wale wasioolewa wameelekezwa kuwa nywele ndefu, zilizomwagika na zilizojisokota.

Wanaume pia wana mitindo yao 14 iliyoidhinishwa na serikali ya nchi hiyo.

Wanaume wamekatazwa kufuga nywele zaidi ya sentimita 5 au nchi mbili wakati huo huo wazee/watu wazima wameruhusiwa kufuga nywele kwa urefu usiozidi sentimita 7 (nchi 3)

Inaelezwa kuwa sheria hii imeleta usawa katika mitindo ya nywele baina ya wanawake na wanaume nchini Korea.

Mwaka 2005 gazeti la Daily Mail liliwahi kuripoti kuwa televisheni ya Taifa ya Korea iliandaa vipindi maalumu vya muendelezo (series) vinavyoelekeza namna ya ukataji wa nywele na mitindo mbalimbali ya ukataji nywele kwa style ya kisasa ya kijamaa.

Lakini mwaka 2017 gazeti la Daily Mail liliripoti tena kuwa katika nchi ya Korea Kaskazini wanawake wana style 15 za mitindo ya nywele na wanaume pia wana style 15 za mitindo ya nywele.

Katika aina hizo za mitindo ya nyweke kuna aina mbili za unyoaji ambazo zimewekwa kwa kundi maalumu.

Katika mitindo hiyo kuna mtindo maalumu wa nywele ambao unanyolewa na kingozi wao nchi hiyo tu Mwenyekiti Kim Jong Un na kuna mitindo kwa ajili wanajeshi, walimu, wanafunzi na kundi maalumu la viongozi n.k.

Iliwahi kuripotiwa kuwa mwaka 2015 Kim Jong Un aliwaagiza wanaume kuiga mtindo wake wa lakini akiweka angalizo kuwa nywele hizo zisikue kuzidi urefu wa sentimita mbili.

Zaidi ya hilo angalizo lilitolewa kwa wakorea Kaskazini kutoiga style ya nywele au unyoaji wa Kibepari.

Je utapenda nchi yako iweke sheria maalumu ya mitindo ya nywele kwa jinsia zote?

Makala hii imeandaliwa kwa Msaada wa vyanzo mbalimbali.

🤣🤣🤣🤣
06/06/2022

🤣🤣🤣🤣

Je ni kweli Nelson Mandela alifia gerezani mwaka 1985?🤔🗣Habari zenu wadau, katika pitapita zangu nimekutana na machapish...
04/06/2022

Je ni kweli Nelson Mandela alifia gerezani mwaka 1985?🤔

🗣Habari zenu wadau, katika pitapita zangu nimekutana na machapisho mengi ya watu wa afrika ya kusini yanayodai kuwa mtu anayefahamika kwa jina la Nelson Mandela, si huyu tuliye mfahamu sisi, Nelson original alifia jela mwaka 1985. Kwa mujibu wa maelezo nikwamba huyu tuliye mzika sisi hivi karibuni ama tuliye mfahamu hakuwa Nelson mwenyewe. Makaburu waliamua kutafuta mtu anayeendana naye kidogo na alilazimishwa kutoa talaka kwa Winnie Mandela maana wangekaa pamoja mwanamama huyu angejua kuwa huyu jamaa hakuwa Mumewe Original.

Inasemekana mwanamuziki Johnny Clegg alishawahi pia kuimba kitu hiki katika wimbo wake wa "Asimbonanga" yaani hatujamwona yeye. Kwenye wimbo huo kuna maneno Asimbonang' uMandela thina akimaanisha hatujamwona Mandela Laph'ekhona - mahali alipo Laph'ehleli - mahali alipo zikwa. Wimbo huu ulitoka mwaka 1987. Ikumbukwe South Africa ilitoka amri kuwa ni marufuku kukutwa unasikiliza ama una miliki album zenye nyimbo za Jonh Clegg, tangu kipindi cha makaburu mpaka kipindi cha mandera huyu aliyetoka gerezani. Maana ngoma za jamaa huyo zilikuwa zinahamasisha harakati za kupinga ubaguzi.

Nani aliyetolewa gerezani 1990?

Inasemekana ni mtu ajulikanaye kwa jina la Gibson Makanda, ambaye alipelekwa katika gereza la Pollsmor mwezi May mwaka 1985. Akiwa huko alifanyiwa plastic surgery iliyofanywa na timu ya madaktari wachache toka London Uingereza. Mara baada ya zoezi hilo kufanikiwa alipatiwa mazoezi ya kuongea na kutembea k**a Nelson Mandela mpaka alipo fuzu ndipo mpango wa kumtoa ukatekelezwa. ndomaana hata baada yakutoka alilegeza sana masharti kwa watu weupe. na aliamua kuunda tume ya msamaha. Ambayo iliwapa nafasi makaburu kutubu waliyowafanyia wazulu kwenye hadhara.

Kwa hivyo kundi hili la watu wanaoamini katika njama hii wanaona uwezekano mkubwa sana kwamba Nelson Mandela lazima aliuawa wakati wa maandamano, na kwamba serikali ya Makaburu Afrika Kusini ilijibu kwa kuwapa mfano ili kuzuia maandamano mengine kwa kuwa walijua aliyekufa alikuwa kiongozi mpendwa na mtu mwenye ushawishi mkubwa.

Inasemekana jamaa baada ya kumpa taraka mama Mandera alitokea kumpenda mke wa raisi wa msumbiji, Samora Machel. Ndio maana baada ya raisi huyo kufariki mchizi akaamua kumuoa mama Machel. Mama akashika rekodi ya kuwa mke wa raisi katika nchi mbili tofauti. Pia usisahau kuwa msumbiji kwa Samora Machel ndipo kulikuwa na kambi ya kikundi cha wapiganaji wa South Afrika waliokuwa wanapinga serikali ya Makaburu, Maarufu k**a Umkhonto we Sizwe(Mkuki wa taifa).

Nilipitia pia vyanzo mbalimbali mtandaoni nikakutana na zaidi ya waandishi 50 tofauti wakizungumzia juu ya Gibson Makanda kuigiza k**a Nelson Mandela. mwaka wa 2018 wakati programu maarufu ya Android inayoitwa Face App ilitolewa. Programu hii inaweza kuonyesha nyuso za watumiaji jinsi watakavyokuwa katika siku za usoni (athari za uzee). Mtumiaji wa Twitter alitumia picha ya ujana inayopatikana ya Nelson Mandela na ​​kuifanyia kazi, akitumia athari ya uzee na matokeo yalionekana kuwa tofauti na sura ya Nelson Mandela katika miaka yake ya hivi majuzi kabla ya kifo.
🗣
Je, nikweli Nelson Mandela alifariki mwaka 1985?🤔

Katika nchi ya Italy, Ottorino Barassi anafika ofisini kwake na moja kwa moja anaenda katika 'vaux', yaani chumba au kab...
04/06/2022

Katika nchi ya Italy, Ottorino Barassi anafika ofisini kwake na moja kwa moja anaenda katika 'vaux', yaani chumba au kabati maalumu kunamohifadhiwa vitu nyeti au vyenye thamani. Vaux ni mahali salama ambapo si rahisi kwa mtu yeyote kuingia na kuiba.

Kwa umakini na usiri mkubwa, Ottorino Barassi anafika katika 'vaux' na kulichukua. Kisha anaenda nalo nyumbani kwake na kulificha. Yote hiyo ni kwa sababu hakutaka kuona wanajeshi wa n**i wanakuja kulichukua.

Ilikuwa ni katika vita ya pili ya dunia, ambapo majeshi ya N**i, yakiongozwa na Adolf Hi**er walikuwa wakilitafuta kwa udi na uvumba ili wapate kulitia mkononi.

Walifika hadi nyumbani kufanya upekuzi lakini hawakuweza kulipata. Kumbe Barassi alikuwa amelificha uvunguni mwa kitanda anacholala.

Unajua ni kitu gani nazungumzia hapo?.

Ni Kombe la dunia. Hi**er alitaka kulinyakua kinguvu mnamo 1939, mwaka mmoja baada ya taifa la Italia kushinda michuano ya mpira wa mguu.

Kombe hilo lilikuwa likiitwa Jules Rimet, likipewa jina la aliyekuwa rais wa kwanza wa FIFA. Ottonio Barrasi alikuwa ni rais wa chama cha soka nchini Italy

Mfahamu Kim Jong Un: Kiongozi Anayendeleza Ubabe Kutoka kwa Babu Zake wa Kale!Denis Mpagaze_____________________________...
27/05/2022

Mfahamu Kim Jong Un: Kiongozi Anayendeleza Ubabe Kutoka kwa Babu Zake wa Kale!

Denis Mpagaze
_______________________________

Wakati mwingine tunaweza kumlaum mtu kwa ujinga alionao kumbe ni ishu ya ukoo wake maana maji hufuata mkono. Sina maana kwamba Kim Jong Un hana akili. Hapana Kim ana akili nyingi tu isipokuwa nazungumzia asili ya ubabe wake. Amerithi kutoka kwa mababu zake. Tangu karne ya kwanza akina Kim walisumbua sana ukanda huo wa rasi ya Korea.

Nakumbuka hata aliyeziunganisha dola hasimu za Goguryeo, Baekje na Silla katika ardhi ambayo wanaamini vurugu, ubabe na vitisho ndio kipimo cha akili kuwa nchi moja ya Korea ni Jenerali Kim Yu-shin. Wanautamaduni wa ajabu. Huko kiongozi mwenye jeshi dhaifu hana akili. Imekuwa hivyo tangu tangu mwaka 57 BC mpaka leo.

Ndiyo maana watu wa ukanda huo ni kutunishiana misuli tu. Wanaamini heri kuogopwa kuliko kupendwa. K**a ni mfuasi mzuri wa tamthiliya za Korea hasa ile ya Jumong utakuwa utaelewa hiyo tamaduni vizuri. Ni tamaduni ya jino kwa jino.

Dola iliyoibuka kuwa imara ilishambuliwa. Babu zake Kim walijenga dola imara ya Silla ikaja kusambaratishwa na dola ya Goreyo baada ya miaka 267. Inatamkwa Kyoreo na siyo goreo. Hii ndiyo dola iliyokuja kuitwa Korea. Ni baada ya wazungu kushindwa kutamka Kyoreo, wakatamka Korea likapita.

Korea iliendelea kuwa nchi moja mpaka pale ilipoangukia kwenye mikono ya Marekani na Urusi 1948. Kwahiyo Kim Kiduku kumtunishia misuli Marekani usidhani maigizo! Jamaa yuko serious sana. Anatekeleza agenda ya wazee wake. Ubabe! Na Marekani akicheza atapigwa k**a alivyopigwa huko Cuba, Somalia na Vietnam. Kim hajawahi kuwa mdogo.

Usicheze na huu uzao wa dhahabu. Unaitwa uzao wa dhahabu kwa sababu babu yao wa kwanza aliokotwa porini akiwa kafungashwa kwenye boksi la dhahabu.
Nadhani mama yake alimzaa na kumtupa porini k**a wanavyofanya wanawake wasuopenda uzee kutupa watoto wao chooni. Hii dunia ni ngumu nyie.Ipo siku tutaamka tusiikute.

Waziri mkuu Mkuu wa Dola ya Silla, Hogong ndio ndo aliliona boksi hilo wakati anapita zake msituni. Alipokwenda kulichukua na kulifungua akakuta kitoto cha kiume kimelala humo, akakipeleka kwa Mfalme Talhae wa Shilla; Mfalme akakipa jina la Kim Al-ji yaani dhahabu.

Sifa ya dhahabu ikipita kwenye moto inang’aa sana, ndiyo maana hawa jamaa wanaamini moto wa vita na vurugu vinawang’arisha sana. Hata hii kutest makombora ya nyuklia ni mwendelezo wa kutaka kung'ara.

Hata baba wa taifa la Korea ni babu yake Kim Kiduku. Namuita Kim Kiduku kwa sababu ya mtindo wake wa kunyoa. Tanzania mtindo huo unaitwa Kiduku. Yeye jina lake ni Kim Jong Un. Natumia Kim Kiduku kuchangamsha makala. Asante!

Babu yake Kim Kiduku aliitwa Mzee Kim Il-sung. Huyu naye alikuwa pasua kichwa. Alianza kupingana na wazazi wake kuhusu kusali bado ni mtoto. Alikataa kuburuzwa k**a sisi tunavyowaburuza watoto wetu kwenda kanisani. Mtoto asipoenda kusali tunampiga badala ya kumuuliza kwa nini hataki kusali. Matokeo yake ndiyo haya makanisa kujaa wahuni, wezi na washenzi.

Enzi za utoto wake huyu Kim Il-sung alimuuliza mama yake kwa nini wanakwenda kanisani kila Jumapili? Mama akasema tunakwenda kurelax, na kweli kila wakifika kanisani mama yake alisinzia na kuamka mwisho wa ibada. Dogo akasema yaani tunakwenda kanisani kurelax na wakati nchi iko kwenye machafuko?

Akasema huyu Mungu wa Kanisani hawezi kuikomboa Kora, ni bora yeye ndio awe Mungu aikombe nchi yake. Unaona hiyo reasoning? Wakati huo Korea inatawaliwa na Japan.

Ndoto yake ya kuikomboa Korea ilianza kuchipua kipindi wazazi wake wamekimbilia China baada ya vita kupamba moto. Huko China Kim akiwa na umri wa miaka nane akaanza harakati za kuikomboa nchi yake hadi akafanikiwa, akawa Rais wa Korea Kaskazini, akapiga marufuku dini na kisha kujitangaza yeye kuwa Mungu wa Korea ndiyo maana hadi leo Korea hakuna dini.

Kila tarehe 15 Aprili, Korea Kaskazini wanaadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Mungu wao; Mzee Kim Il-sung. Na huwa ni sherehe kubwa k**a Krismas na Idi. Kuanzia asubuhi mpaka jioni maelfu ya watu humiminika kwenye jumba la makumbusho alikolala huyo Mungu wao. Amekaushwa vizuri. Hakuzikwa. Ukifika unamuona. Anafanana sana na Kim Kiduku. Au unaweza kumuita Kim Masuruali. Suruali zake ni pana k**a lile dude la kutolea unga mashineni. Fundi wake ni jasiri sana.

Siku hiyo TV zote huonyesha matukio ya Kim Il-sung akipigana msituni kuikomboa Korea kutoka kwa Wajapan. Wajapani waliivamia Korea mwaka 1905 baada ya kumshinda Urus katika ile vita ya Japan na Urus iliyoanza mwaka 1904 hadi 1905.

Japan ilikuja kuipoteza Korea baada ya kushindwa kwenye vita ya pili ya dunia. Ni baada ya Marekani kuitwanga Japan mabomu ya nyuklia pale Hiroshima na Nagasaki. Korea ikawekwa chini ya uangalizi wa wababe wawili wa dunia Urus na Marekani.

Kwa sababu fahari wawili hawakai z**i moja ikabidi Korea ipigwe pasu. Marekani ikachukua Kusini na Urus ikichukuà Kaskazini. Joseph Stalin akampa Kim Il-sung nchi ya Korea Kaskazini. Kim akaivamia Korea Kusini mwaka 1950 ili kuunda taifa moja la Korea,lakini akashindwa maana alikuta Marekani kadinda pale. Vita ikaisha mwaka 1953. Hadi leo Korea Kusini ni mali ya Marekani. Gusa unuke.

Ikabidi Kim Il-sung aelekeze hasira zake kwenye ujenzi wa nchi kwa falsafa ya kijamaa. Uchumi wa Korea Kaskazini ukakua kwa kasi hadi ulivyodumaa miaka ya 90 kutokana na ukame na kuvunjika kwa USSR.

Mwaka 1994 Mzee Kim alikufa. Mwanaye Kim Jong Il, baba wa huyu Kim Kiduku akashika nchi. Huyu naye alikuwa mtata halafu mpenda movie.Alikuwa na studio ya filamu kabla ya kuwa kiongozi. Lakini pia alikuwa na maktaba ya muvi 20,000 za Hollywood na aliwahi kuandika kitabu cha sinema. Leo tamthiliya za Kikorea zinawamaliza akili dada, mama na wake zetu.

Kitaaluma Kim Jong Il ni rubani wa ndege. Alisomea huko Ujerumani Mashariki kwa miaka miwili. Aliingia ikulu na sera yake ya Jeshi Kwanza , Marekani wakash*tuka. Huyu kichaa vipi? Mwaka 2002 George W. Bush akaiweka Korea kwenye kundi la nchi za kishetani, yaani Axis of Evil. Nchi nyingine ni Iran na Iraq lengo amle kichwa.

Huwa tunasema ukitaka kumuua mbwa wako mpe jina baya. Korea Kaskazini, Iran na Iraq wakapewa jina baya. Wanahatarisha usalama wa dunia kwa kutengeneza nyuklia. Wakaishia kumuua Saddam Hussein ambaye hakuwa hata na hizo silaha za nyuklia.

Korea akawaambia k**a nyie ni wanaume niguseni. Kim Il-sung akajitoa kwenye Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Nyuklia. Mei 2009 akatest kombora la kwanza la nyuklia. Marekani wakatamani kufa.Wakajifariji kwa hekima za wahenga wa Afrika kwamba ukiona adui yako ananoa panga kila siku basi ujue anakuogopa. Hii siyo kwa Korea. K**a wanadhani anawaogopa waguse tuone.

Bahati yao Marekani Kim akiwahi kufa. Akikufa Disemba 19, 2011 akiwa na miaka 69 kwa ugonjwa wa moyo. Mwanaye Kim Jong-Un akachukua nchi, Marekani wakajua mambo yatakuwa shwari kumbe heri baba. Kim anawanyima usingizi hadi leo. Trump hana hamu.

Halafu Kiduku anawaweza kwa sababu kapata elimu ya Kimagharibi. Amesomea Uswisi. Alipelekwa huko kwa siri akiwa mdogo. Alisoma pale Bern International School kwa kutumia jina feki. Aliitwa Park Un, mtoto wa mwanadiplomasia wa Korea Kaskazini. Acha sisi mtoto wa DC utataka shule nzima ijue.

Somo alilofaulu vizuri ni muziki. Alifeli hesabu na sayansi. Alivyorudi nyumbani aliendelea na masomo katika Chuo Kikuu cha Kivita cha Kim Il-Sung kuanzia mwaka 2002 hadi 2007.

Hadi Kim Kiduku anapewa nchi hakuwa maarufu kabisa. Dogo amelelewa katika mazingira ya usiri sana. Hata umri wake haujulikani mpaka leo. Acha sisi katoto kanazaliwa leo tu full kukaanika mitandaoni kwa sababu hatujui huko mbeleni katakuwa kanani.

Wenzetu mtoto anazaliwa na agenda ya kutekeleza. Wako focused tangu utotoni. Sisi tunaanza kuwa focused umri umekwenda sana ndiyo maana ubabaishaji ni mwingi sana.

Tangu mtoto huyu ameshika nchi yeye na makombora tu. Anayafyatua kwelikweli. Samaki huko baharini hawana hamu. Halafu akiyafyatua anacheeekaaa na fegi mkononi. Februari 2013, alifanyatua kombora la kwanza la nyuklia na baada ya hapo ikawa ndio utamaduni wake kuchangamsha dunia kwa makombora.

Marekani wakasema huyu dogo anajiamini nini? Vita ya maneno vikazuka kati ya Kim na Donald Trump. Halafu ukiangalia umri wa Kim na Trump haviendani kabisa. Ni sawa na mtu na babu yake. Adabu sifuri. Trump ameondoka madarakani hana hamu na Kiduku. Biden ndio kabisa hataki hata kumzungumzia.

Bora tu aachane naye maana bwana mdogo akili zake an**ijua mwenyewe. Anasemaga ni heri kuogopwa kuliko kupendwa. Kim Kiduku bhana. K**a akiua mjomba wake wa damu sembuse wazungu? Alimuua Desemba 2013 . Anko wake aliitwa Jang Song-Thaek. Alimuua kwa kosa la ubadhilifu wa mali ya umma. Alipomaliza kuua akasema ameondoa uchafu kwenye chama. Eti uchafu ndani ya chama.

Hivi akija Afrika siataua wote? Maana huku kuna madudu mpaka unajiuliza hivi sisi kweli ni binadamu halisi au nyani? Haiwezekani mtu unaiba mali za umma hadi unakosa pa kuweka na wakati kuna ndugu zako wamekosa hela ya kusafirisha maiti tukasema wewe ni binadamu. Kwakweli wewe ni myama. Unajilimbikizia mali utadhani utaishi milele. Roho mbaya tu. Ndiyo maana mnakufaga vibaya.

Siku moja Mike Pence, Makamu wa Rais wa Marekani akajichanganya kumtishia Kim Kiduku kwamba asipobadilika yatampata yaliyompata Muammar Gaddafi wa Libya. Kim akawatuma wasaidizi wake wamwambie hana akili. Jibu hilo lilimtishia Trump hadi akaghaili kushiriki mkutano aliopanga kukutana na Kim Jong Un.

Kim akamwambia relax mzee, usiahirishe bana. Trump akakubali. Juni 12, 2018, Trump alikutana ana kwa ana kumbembeleza Kim aachane na silaha za nyuklia. Kim akamwambia niko tayari endapo na nyie mtaacha kufanyia mazoezi ya kijeshi Korea Kusini. Kwani waliacha sasa!

Unajua Marekani wanaoneaga nchi zisizo na vnyuklia k**a Iraq ya Sadam na Libya ya Ghadaffi. Ukiwa na nyuklia wanakubembeleza muwe marafiki tena mpaka hela wanakupa lakini kwa Kim wamedunda.

Angalia Marekani wanavyojikomba Pakistan. Karibu robo tatu ya bajeti ya Pakistan kwenye mambo ya ulinzi wanatoa wao pamoja na kwamba Pakistan anafadhili vikundi vya ugaidi vinavyoua Wamarekani. Marekani wanaogopa Pakistan itawapa nyuklia magaidi wawaangamize.

Hata Korea Kusini wanakula Marekani. Marekani hawezi kutoka Korea Kusini ili aendelee kumdhibiti China isiendelee kujitanua ukanda ule ndiyo maana huwa anafanya juu chini nchi hizo zisiungane. Kinachoonyeshwa kwenye tamthilia ya IRIS ndio uhalisia. Wakorea hawaigizi vitu vya kubuni, sijui Jini limeoa mke wa mtu. Wao wanaigiza uhalisia. Katika Movie ile IRIS ni hila za mabepari kufifisha muungano wa Korea.

Uwepo wa Marekani pale Korea Kusini umewapumbaza Wakorea hadi kutotambuana k**a wao ni ndugu. Wan**inguana kila siku. Ni sawa na sisi Waafrika tunavyoitana maadui na wahamiaji haramu. Eti Mtanzania anamuita Msomali muhamiaji haramu. Kwakweli wazungu walituweza.

Ila kinachonifurahisha kwa Wakorea Kaskazini ni uzalendo wa kusimama na nchi yao. Hawakengeuki ng’oo. Pamoja na viongozi wao kushambuliwa kwamba ni madikteta wao wanawapenda mpaka basi. Ushahidi mzuri ni siku ya msiba wa baba yake Kim Kiduku. Watu waligalagala barabarani wakimlilia dikteta wao. Dunia iliwashangaa k**a sisi dunia ilivyotushangaa tulivyogalagala barabarani kumlilia Nyerere wakiamini ndio alietuletea umaskini na kutubana sana!

Kwamba Korea Kaskazini watu wanakufa njaa kwa sababu ya udikteta. Mbona hata nchi za kidemokrasia watu kibao wanakufa njaa? Kwamba Wakorea Kaskazini wanavuka mipaka kukimbilia Korea Kusini kutafuta maisha. Hii nayo ni hoja ya kijinga tu. Mbona hata wamarekani wanavuka kwenda Canada na Mexico.

Sikiliza. Kiongozi yeyote ambaye haendani na maslahi ya Wazungu lazima atakuwa dikteta hata k**a wananchi wake wanampenda. Marekani kwenyewe hakuna hiyo demokrasia. Demokrasia gani ya kuua ndugu zetu weusi tu? Juzi tu wameua.

Kwanza hii demokrasia ndio hufanya tuendelee kunyonywa. Kwani demokrasia ya magharibi ni nini k**a siyo kuwa mtiifu na kuitika kwa anayekuibia?

Sasa k**a Korea Kaskazini watu wanakufa kwa njaa mbona hawaishi? Hakuna taifa maskini lenye uwezo wa kutengeneza mabomu ya nyuklia. Wakorea Kaskazini wameamua kuishi kivyao. Hata mambo yao hayajulikani kirahisi. Nchi nzima ni usalama wa taifa. Wanailinda na kuipigania na huo ndiyo uzalendo.

Wakorea wamefanikiwa sana katika kutunza siri. CIA na ushushu wao wameshindwa kuingiza pua zao huko. Hata habari za utengenezaji wa makombora ya nyuklia hawakujua, walikuja kush*tuka yanafanyiwa majaribio. Hao ndo wana intelijensia bobevu. Wamekomaa haswa katika kuficha mambo yao k**a Afrika tumevyokomaa katika kuficha wezi. Tunaibiwa mchana kweupe na hakuna anayetoa siri za wezi. Bure kabisa.

Wakorea ndiyo wajamaa wa kweli na wenye kustahili kuitana makomredi. Siyo huko kwenu hata wezi wakubwa wanaitana makomredi. Ajabu sana! Ndiyo maana wajamaa wanatuchukia Arika. Wanatuita ndumilakuwili. Mwizi anajiita mzalendo.

Wakati wa vita baridi nchi za kijamaa walituamini sana lakini kwa tamaa zetu tukawa tunauza habari zao kwa maadui mpaka maadui wao wakashinda.Tunajiita eti hatufungamani. Tuko nutro ili tule. Ndio maana hata sasa hivi Wachina hawana huruma na Afrika kwa sababu tuliwarudisha nyuma sana.

Kuna mengi ya kujifunza kutoka Korea tuyachukue. Kule bwana kila kitu ni kinasisimua. Kule ukiwa na mchepuko unatambuliwa kiserikali na unapewa huduma zote. Watoto ni watoto pia. Hawana cha mtoto wa nje. Watoto wote ni sawa. Hata huyu Kim Jong Un ni mtoto wa nje. Hii ni meseji nzuri kwa wenye watoto wa nje. Hebu watunzeni vizuri maana yawezekana hao ndio wamebeba baraka za ukoo wako. Unaweza kupendelea watoto wa ndani ndio wakaja kukuua.

Kuna watu wanadhani ni sound. Baba Kiduku alioa wanawake wawili na mahawala watatu.Mahawala wenyewe ni Song Hye-rim, Ko Yong-hui yaani mama yake Kiduku na hawala wa tatu ni Kim Ok. Mke wa kwanza Bi Hong il-Chong alizaa mtoto mmoja wa k**e, Kim Hye-gyong, mke wa pili ni Bi Kim Young-sook, alizaa mtoto mmoja wa k**e, Kim Sul-song na hawala wa kwanza yaani Bi Song Hye-rim alimzaa Kim Jong-nam.

Sasa katika orodha ya watoto wake wote hao mtoto mkubwa wa kiume ni Kim Jong-nam kutoka kwa hawala yake wa kwanza. Huyu ndo alitakiwa kumrithi baba yake lakini ilikuja kubainika alikuwa wakala wa CIA, vyombo vikamtema. Wakati huo Kim Jong-nam akiishi zake China kwa posho ya CIA. CIA walijua dogo atapewa nchi wakamrob ili aiuze kwa mabepari k**a alivyofanyaga Mikhail Gorbachev kuuza Umoja wa nchi za Kisovyet.

Mwaka 2010 mzee akatangaza rasmi kwamba Kim Jong-Un ndiye mrithi wake na mwaka 2011 mzee alilala. Kim Jong-Nam alipopata taarifa za kifo cha baba yao alikwenda Korea Kaskazini na kukutana na mdogo wake Kim Kiduku.Kiduku alimuona kaka yake k**a kiwingu, hivyo akapanga kumuua baada tu ya mazishi. Bro aliposikia akarudi zake China kabla dogo hamjatoa roho kwa mali za baba yao. Hakuzika.

Baada ya mazishi Kim Jong-Un akapewa nchi rasmi na kuendelea kumsak**a kaka yake Kim Jong-Nam ili amuue. Kim Jong-Nam aliposikia Bwanamdogo anamuwinda aliamua kumuandikia barua kumuomba asifanye hivyo. Hata hivyo Februari 13 mwaka 2017 Kim Jong-Nam aliuawa kwa sumu akiwa uwanja wa ndege wa Kualar-Lumpar, Malaysia akisubiri ndege kurudi zake China. Vibinti viwili vilivyovalia gloves vilimshika usoni na kutoweka. Dakika chache hali yake ilibadilika na alipokimbizwa hospitali alifariki dunia.

Huyo ndiyo Kim Jong Un, small guy but tough in decisions. Hanaga msamiati huruma. Kim anaamini kuwa k**a haiwezekani ukaogopwa na kupendwa kwa wakati mmoja, basi ni heri uogopwe kuliko ukapendwa.

Kim Kiduku anamuamini dada yake wa tumbo moja tu. Anaitwa Kim Yo Jong. Alizaliwa 26 Septemba, 1988. Wamelelewa sehemu moja na wamesoma wote Uswiss. Binti anadigrii ya sayansi ya kompyuta.

Kim akiwa kwenye matibabu huwa anamuachia nchi huyu dada. Kim amekua mtu wa kuugua mara kwa mara ingawa taarifa za ugonjwa wake ni siri. Hata akisafiri kinyesi chake kinatunzwa. Hanyi hovyo.

Wanasema anaugua hovyo kwa sababu napenda kula kula vitu vyenye sukari nyingi k**a vile p**i na wine. Halafu anapiga sana fegi. Fegi kwao na nature. Hata baba yake alikuwa mpiga fegi mbobevu. Enzi za uhai wake alitumia sigara aina ya Rothman yenye tumbaku asilia kutoka Afrika.

Mara nyingi Kiduku anaongozana na huyu mdogo wake. Naskia akifa huyu dada ndio anachukua nchi maana watoto wa Kim bado wadogo. Ila mie naomba Kim kiduku asife bana. Kiduku anaichangamsha dunia maana tangu Osama bin Laden atutoke ilikuwa imepoa sana. Mie Kim ananifanya nisijihisi mpweke hasa kipindi hiki cha bei mafuta kupanda bei! Oya mwanangu Kidukuu! Watu wa Musoma tunakuelewa sana kaka!

Kwa sasa huyu binti ndiyo anasimamia like kundi la ujasusi uliopitiliza. Linaitwa Room 39. Lilianzishwa kwa lengo la kuhakikisha viongozi wa Korea Kaskazini hawakosi fedha za kigeni. Iwe kwa haramu au halali kikubwa pesa ipatikane na viongozi wao wasikwame.

Kitengo kimesheheni majasusi wenye akili kubwa kutoka kila sekta. Ukizungumzia wataalam wa kufoji pesa ndio mahali kwao. Wamewahi kufoji dola ya marekani ikatumika miaka zaidi ya ishirini bila Marekana kujua. Imagine hadi zikaitwa The Super fake Dollars''. Marekani walivyogundua ni Wakorea jamaa walikana hadi leo.

Marekani wakajaribu kubadilisha dola lakini ikafojiwa tena. Na pesa yao inasambaa dunia nzima halafu mtu anasema hawa jamaa wanakufa njaa. Hizi habari wadanganyeni hao waliojikalia k**a furushi la mitumba kusubiri kuletewa kila kitu. Siyo sisi wafukunyuzi.

Hawa watu wenye macho madogo na sura pana wana akili nyinyi aisee. Nikikwambia bidhaa za Marekani zinauzwa dunia nzima huwezi amini. Unajua wanafanyaje? Wanatengeneneza bidhaa halafu wanapiga lebo ya China, mzigoo unaingia sokoni. Kazi ya Majasusi wa Room 39 dadake.

Hawa jamaa ni fisi! Mwaka 2016 walidukua hadi hazina ya Marekani na kuchota dola bilioni 1. Waliwahi kuingia kwenye mifumo ya ulinzi wa anga ya Korea Kusini na kuiba ndege za kivita na kuondoka nazo jumla. Vijamaa ni vidogodogo lakini kwa akili loh!

Kwa matango pori sasa loh! CNN hawana hamu! Kuna siku waliimbia CNN Kim Jong Un amekufa, vyombo vya habari vyote vya magharibi vikaingia cha k**e. Wiki moja baadaye Kim akaonekana akiwa anakata utepe kwemye kiwanda cha mbolea, baada ya hapo akatest kombora moja, akatulia zake. Jamaa wanakeraa!

Januari hii 2022 ndiyo alifanya kufuru. Amefanya majaribio saba mfululizo. Humo amerusha kombora jipya la hypersonic. Lina uwezo wa kusafiri zaidi ya mara kumi ya spidi ya sauti. Kila akilipua utasia, badala alishe watu wake anaharibu kwenye makombora. Hizo ni akili zinazowaza kula.

Halafu unamshangaa Kiduku kwamba anatumia pesa kwenye makombora badala ya kununua chakula lakini haujishangia wewe unayeshinda njaa ili upate bando la kuangalia makombora yake. Sikiliza! Maisha ni kuchagua. Ulichonacho hakinihusu. Weka jiwe niweke shoka!

Wakati nchi zetu zinaogopa kusema chochote kuhusu vita ya Urus na Ukraine, Kim aliunga mkono hadharani. Jamaa yupo deep sana kwenye vurugu k**a hizi. Namuona kwa mbali anaimezea mate hiyo vita. Tunasubiri salam k**a za Kiduku kutoka Irani, Syria na China.

Kim anakwambia hata hilo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni genge la walaji. Wamejipa viti vya kudumu Anasema halipaswi kuitwa Baraza la Usalama bali linapaswa kuitwa baraza la kigaidi. K**a hujui historia ya Kim unaweza kusema ni mvuta bangi. Kwamba hana akili. Hivi nani kakwambia wavuta bangi hawana akili? Asiye na akili ni yule kijana anayetamani Putini na Kim waje wampe msaada kwenye penzi lake.

Nimesikia corona imeingia Korea Kaskazini. Hofu yangu asijekuwaua wagonjwa. Maana ameisha wageuka madaktari.Kwamba wamefanya uzembe mkubwa. Waziri wa afya anapumulia juu. Oxyegen haitoshi.

Wacha tuishie hapa kwa leo tujiandae na historia ya Putin....kumekucha!

Jipatie vitabu vyangu kwa bei ya Sh 5,000 kwa kila kimoja. Ni softcopy. Mpesa 0753665484. Vitabu ni Ukombozi wa Fikra; Maisha ni Kutafuta Siyo Kutafutana; Viongozi Wanaoishi Baada ya Kufa na Ukombozi wa Fikra za Mwafrika. Ukitaka kuwa wakala wa vitabu vyangu Mpigie Chaula, bahiri wa taifa +255753690907

Wako
Mwl.Denis Mpagaze
Muhenga wa Karne ya 21Mfahamu Kim Jong Un: Kiongozi Anayendeleza Ubabe Kutoka kwa Babu Zake wa Kale!

Muhenga wa Karne ya 21

Address

Nyegezi

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when JE WAJUA. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to JE WAJUA.:

Share