23/12/2021
Imeandikwa
Ndugu yangu
Faraji Buriani Nandala
Tukielekea kuumaliza mwaka 2021,kwangu mimi mwaka huu ulikua ni mwaka wa mapambano zaidi,mapambano ya kutimiza malengo ya muda mrefu ya kumiliki kampuni yangu binafsi.
Ni mwaka nilio timiza moja ya ndoto yangu ya muda mrefu ya kumiliki kampuni yangu binafsi ,Haya ni matokeo ya changamoto nyingi nilizo kutana nazo kwenye maisha yangu ya kuajiliwa kwenye taasisi mbalimbali.
Changamoto nilizo kutana nazo kwenye taasisi mbalimbali nilizo wahi kufanya kazi,zilinifanya nikomae kiakili na kunipa matamanio ya kujiajili mimi mwenyewe na ikiwezekana nitoe ajira kwa vijana wenzangu wanao angaika kila siku kutafuta ajira.
Inshaallah mwenyenzimungu amenibariki nimefanikiwa kusajili kampuni yangu binafsi ya ulinzi inayo itwa RESPECT SECURITY SOLUTIONS COMPANY LIMITED Respect Security Solutions Company Limited . Hii ni kampuni binafsi ya ulinzi iliyo sajiliwa kisheria na kupata ithibati ya kisheria ya kufanya shughuli za ulinzi binafsi kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makao makuu ya kampuni hii yako Masasi Town Council mtaa wa Jiddah karibu kabisa na ofisi za Mohammed enterprise.Kampuni hii kwa sasa inatoa huduma zote za ulinzi kwenye ofisi na taasisi mbalimbali za kiserikali na binafsi.Huduma zetu ni bora,za kisasa na zenye kuzingatia matakwa ya wateja na zinazo Linda maadili na tamaduni za kitanzania.
Gharama zetu ni nafuu zinazo tozwa kulingana na mahitaji na matakwa ya wateja wetu.Kampuni hii inavijana imara,wakak**avu na wenye nidhamu waliopata mafunzo kutoka jeshi la kujenga Taifa(JKT) na Jeshi la Akiba yaani Mgambo.Vijana hawa wamedahiliwa na kuchujwa kwenye chujio maalumu na kisha kuwapata vijana walio bora katika shughuli za ulinzi.
Kwa sasa tunatoa huduma za ulinzi kwenye ofisi mablimbali(ofisi binafsi na serikalini),tunatoa huduma za ulinzi kwenye viwanda,maghala,nyumba binafsi na kusimamia sherehe na mikutano mbalimbali. Kwetu mteja ni mfalme na tunaamini kwa pamoja tunaweza kuuweka ulimwengu kua sehemu salama ya kuishi.
Karibu tukuhudumie,
Karibu Respect Security Solutions Company Limited.
Ahsante.
Ndimi,
Faraji Buriani Nandala
Owner,CEO,Managing Director
Respect Security Solutions Company Lim