Riwaya na Hadithi

Riwaya na Hadithi Bookstore

DEAR PESA____________Mpendwa pesa, ni nini nilichokukosea? Mbona umejitenga na kuwa mbali ya upeo wa  macho yangu? Niwek...
24/04/2024

DEAR PESA
____________
Mpendwa pesa, ni nini nilichokukosea? Mbona umejitenga na kuwa mbali ya upeo wa macho yangu? Niweke wazi ili nielewe.

Labda mimi ndiye mkosefu kwako, lakini mbona kumbukumbu zangu hazioneshi nilichowahi kukukosea.

Iwapo kunalo jambo lililokukera kwangu naomba uliweke wazi nitambue. Mie nikitakacho ni mimi na wewe kumaliza tofauti zetu.

Mwanzo ulipokaa kwangu siku tatu nilidhani huenda ndio umekuja mazima na hautaondoka tena. Kitendo chako cha kuondoka ghafla kiliniletea msongo wa mawazo. Kidogo hata nijinyonge k**a sio huyu jirani yangu kukata kamba. Mimi nililala nilipoamka sikukukuta. Mpaka leo sijajua chanzo ni kipi.

Ni nini ulichoona kibaya kwangu mpendwa pesa mpaka hutaki kurudi?

Au ulishajua kuwa ukiishi kwangu nitabadilika nijae majivuno na dharau. Ama uliona sina sehemu ya kukuhifadhi?

Mpendwa pesa.......
Nimeshapata habari kuwa wanafiki walikujaza maneno eti nimekutukana. Lakini ukweli ni kwamba wala sikukutukana, mimi nilipita tu nikasikia wakikusema vibaya, kuwaβ€”eti wewe pesa ni shetani. Basi mimi nikaamua kukutetea, nikakataa na kukataa kuwa wewe sio shetani bali malaika mwema mtatuzi wa changamoto. Hapo nilifanya makosa?

Mpendwa pesa.. ...
Kila siku naisafi mikono yangu ili angalau siku ukirejea nikushike bila kukuumiza. Labda mikono yangu yenye gaga mithili ya wembe ndiyo unayoihofu. Lakini mbona miezi yakatika pasipo dalili yako?

Ama waleti yangu inatoa harufu mbaya inayokufanya ushindwe kurudi ukiikumbuka? Au ni kadi zangu za benki zisizo hata na ndururu ndizo unaziziogopa huku ukiona utakuwa mpweke kuishi ndani yake?

Mpendwa pesa.......
Mimi bado nakupenda! Ushakwenda tezi na omo, basi rejea ngamani tuanze ukurasa mpya niache kunung'unika.

Au iwapo hutaki kurejea leo mtume hata mwakilishi wako aje kunipooza kwa hizi shida nilizo nazo wakati wewe ukifungasha mafurushi yako ili uje jumla.

Mpendwa pesa.....
Nimekumiss hakika. Siku zote nataabika, Sina hata pa kushika. Hebu rudi malaika, niache kuhangaika! Ukweli wazi naweka, toka ulipoondoka chakula hakijanishuka. Hali yangu ya mashaka, sina shoka wala shuka.

Nipo tayari kukulaki k**a upo warudi. Iwapo kuja hutaki nasema tupo tunaingia site kukutafuta mimi na wanangu. Tumeshajua ulipo.

Marwa

23/11/2023

WAIVU

Waivu mnayo kazi, vibomu kwami njiani,
Anihusudu mwenyezi, kazi kwenu shindaneni,
Ni bure wenu ulozi, tafuta kazi fanyeni.

Mizizi mtamaliza, na mahirizi mwilini,
Mwisho mtajilemaza, muache chuma vijani,
Mie shida mwanchagiza, walimwengu mwatakani.

Mwiba kwenu siha njema, lengo niwe mahamumu,
Hamtaki kunitema, kwani nyiye mahakimu,
Vijini vyenu mwatuma, vije kwangu kujikimu.

Hebu basi nitueni, k**a koma nikomeni,
Siutaki ushindani, vigagula sikieni,
Nachotaka niacheni, hamsini zishikeni.

19/11/2023

Chogo kaona bora ajiue mwenyewe

19/11/2023
π‘πˆπ–π€π˜π€: πŒπ–πˆπ™πˆ πŒπ–π€ππƒπˆπ’π‡πˆ:   Marwa Patrick        π’πˆπŒπ”: πŸŽπŸ•πŸ’πŸ”πŸ’πŸπŸ”πŸ—πŸ•πŸ‘                        π”π“π€ππ†π”π‹πˆπ™πˆ Kitendo cha kujifungu...
03/08/2023

π‘πˆπ–π€π˜π€: πŒπ–πˆπ™πˆ
πŒπ–π€ππƒπˆπ’π‡πˆ: Marwa Patrick
π’πˆπŒπ”: πŸŽπŸ•πŸ’πŸ”πŸ’πŸπŸ”πŸ—πŸ•πŸ‘


π”π“π€ππ†π”π‹πˆπ™πˆ

Kitendo cha kujifungua mtoto akiwa ametanguliza miguu badala ya kichwa kilimpa msh*tuko sana. Mawazo yakaanza kumwandama kichwani mwake. Alifikiri kuwa huwenda kuna mchawi alikuwa akimchezea. Itakuwaje ajifungue mtoto akiwa ametanguliza miguu? Mawazo hayo yalimwandama kwa sababu alikuwa anajua kuwa kwa mila za jamii yao mtoto aliyezaliwa akiwa ametanguliza miguu aliaminika kuwa ameleta mikosi na laana kwenye familia au jamii husika. Kiufupi ni kuwa anazaliwa akiwa anailaani dunia. Na kwa utaratibu uliokuwepo ni kwamba mtu wa namna hiyo alikuwa akitengwa na jamii au familia yake.

Alipowaza kwa muda alikumbuka kuwa hakuna mtu mwingine ambaye alikuwa anajua kuwa mwanae amemzaa kwa namna hiyo. Ni yeye tu aliyekuwa anajua hilo. Hivyo aliapa kuwa jambo hilo angelihifadhi moyoni mwake iwe siri yake mwenyewe. Akaapa kutokumwambia hata mme wake ambaye kuonekana kwake kulikuwa kwa nadra sana.

Wakati yeye alipokuwa anahangaika kujifungua bila msaada wowote. Mmewe alikuwa kwa mchepuko wake akihangaika kuupandisha kilele cha raha. Sasa walikuwa wamemaliza robo ya kwanza ya kuupanda mlima huo. Walipumzika kabla hawajaendelea ili kukamilisha sehemu iliyobakia. Kisha waliianza safari yao ya kuupanda mlima huo. Mlima wa raha usiofikika kimwili bali kihisia.

Hatimaye, baada ya jasho jingi kuwavuja wakawa wamekifikia kilele. Sekunde kadhaa walizobaki hapo zikawafanya wajione k**a wako peke yao duniani. Huko hata hawakukaa sana wakawa tayari wameshuka.

Herbert alikuwa amezama ndani ya penzi zito la Simiat. Mwanamke ambaye hakuwa na mme wala mtoto. Mme wake alifariki yapata mwaka mmoja uliopita kwa maradhi ambayo hayakujulikana. Toka hapo hakutaka kuolewa tena licha ya wanaume wengi kumtaka. Mwanzo aliapa kutokuwa na mwanaume yeyote wa kudumu ila alijikuta akiangukia kwa Herbert. Aliposh*tuka tayari mimba changa ilikuwa ikikua taratibu tumboni mwake. Basi tangia hapo akaamua kuwa iwe isiwe lazima Herbert ailee mimba mpaka mtoto akue.

Simiat alifikiri namna ambavyo angeweza kumteka mwanaume huyo ili amfanye mme wake japo alijua kabisa kuwa alikuwa mme wa mtu. Ila hakujali hilo, moyoni alijisemea kuwa 'cha mtu huliwa na mtu'. Basi akaongeza mapenzi maradufu kwa Herbert. Yote nikuhakikisha kuwa anamuweka kwapani kabisa.

Mapenzi hayo mazito yakamlevya mme wa mtu. Akaisahau familia yake. Akahamia nyumbani kwa mchepuko. Akawa anaenda kuiona familia yake mara moja moja kwa mwezi. Hata pesa alizokuwa akizipata kwenye gereji yake akipokuwa akifanya kazi hazikumfikia mkewe. Isipokuwa ziliishia kwa Simiat zikitumika kukuza ujauzito mchanga.
Wakati Herbert akijitutumua kukuza mimba changa kwa mchepuko, alisahau kuwa mkewe, Nadina alikuwa mjamzito, tena alikuwa karibu kujifungua.

Mapendo yalikuwa yamekwishamchanganya hakukumbuka kuwa alikuwa na familia. Simiat naye alikuwa mwanamke mjanja sana. Alijua kuwa mapenzi pekee yasingeweza kumfanya amumiliki mme wa mtu. Hivyo akajiongeza na kuamua kuwa ni lazima atumie njia nyingine mbadala ili amteke kabisa awe wake asiwe na kauli mbele yake wala asisikilize ushauri wa yeyote. Ndiposa akaingia katika sayansi ihusishayo mitishamba yenye nguvu asilia k**a yeye alivyoiita.

Simiat alikuwa mtaalamu sana. Hasa kwenye masuala k**a hayo ya kumk**ata mwanaume na kumuweka kiganjani mwake, Kisha akamfanya atakavyo. Alipokuwa unyagoni alifundwa akafundika, akafunzwa akafunzika. Kungwi wake alikuwa mtaalamu haswa katika nyuga hizo. Alifunzwa mbinu mbalimbali za kumpumbaza mwanaume na kisha akamgeuza na kumfanya atakavyo. Mwanaume akawa mshabaha wa kizuu. Yani mwanaume anakuwa k**a roboti anafanya kila anachoelekezwa pasipo kuhoji chochote.

Simiat akiwa ameamua kuyatumia yale aliyofunzwa ili kumfunga kwake Herbert. Alianza kwa kuchagua njia bora zaidi ambayo ingempa matokeo bora zaidi. Njia ambayo pindi itumiwayo ni ngumu kwa mhusika kurudi katika hali yake ya kawaida hata k**a akipelekwa kwa mganga aliye mtaalamu kiasi gani. Basi Simiat akaitisha kikao cha dharura kichwani mwake na kikao hicho kikaanza mapema iwezekabavyo. Hisia zake zote akazihamishia huko ili kufuatilia kila hatua mpaka pale atakapopata jibu la tatizo lake. Muda si mrefu akapata jibu. Jibu hilo aliona kuwa ndilo suluhisho la jambo lililokuwa kichwani mwake. Mara moja akaamua kulifanyia kazi wazo hilo.

Bila kupoteza wakati akasimama kutoka kitandani alipokuwa amekaa. Akainama na kuchungulia uvunguni mwa kitanda kisha akavuta kitu namna ya kimkoba kidogo cha ngozi. Akakifuta vumbi kisha akakifungua akapangua vitu vya aina aina kisha akakipata kile alichokuwa anakihitaji na kukichukua.

Kitu hicho kilikuwa ni kichupa kidogo na alipokifungua ndani kulikuwa na unga mweupe. Akakifunika na kukiweka pembeni kichupa hicho, akafunga kile kimkoba na kukirudisha kilipokuwa na kuondoka kuelekea nje.

Muda huo Simiat alipokuwa anataka kufanya alichokikusudia. Herbert yeye alikuwa njiani akielekea nyumbani kwake. Alikuwa amepata taarifa kuwa mkewe amejifungua mtoto wa kiume. Sasa alikuwa akisubiliwa yeye tu ili mtoto huyo apewe jina. Basi alipofunga gereji yake akaamua moja kwa moja aende mpaka nyumbani kwake pasipo kupitia nyumbani kwa Simiat. Alijua wazi kuwa iwapo angepita huko basi safari ya kwenda kumuona mkewe aliyekuwa amejifungua ingekomea hapo. Alipitia kwenye duka la nguo za watoto akamnunulia mtoto nguo. Kisha akanunua vitu vingine hitajika na kwenda navyo nyumbani.

Alipofika nyumbani alimkuta mkewe amenuna isivyo kawaida. Mkewe naye alipomuona akasonya msonyo mrefu sana. Kisha akakaa tuli akiwa ameangalia pembeni. Kisha muda si mrefu Nadina akaanza kumtapikia maneno baada ya Herbert kujaribu kuyaanzisha mazungumzo.

"Enhee, wewe ni nani kwani? Umetoka wapi? Unataka nini? Kwani huko ulipokuwa umeolewa imekuwaje tena? Usije ukaniambia kuwa umeachika mapema namna hiyo"

"Ah! Maswali gani hayo tena mke wangu? Hunifahamu au dharau? Au umepata kichaa baada ya kujifungua?" Herbert alimjibu mkewe.

"Kwani wewe unatakaje. Si nimekuuliza ili nijue kuwa huko ulipokuwa umeolewa umepewa talaka au imekuwaje? Hii ni wiki ya ngapi toka uondoke hapa? Ukaniacha peke yangu nateseka. Halafu mpaka nimejifungua ukajua ila hukutaka hata kuja kumuona mtoto. Sasa leo kilichokuleta ni nini?"

"Sasa wewe ulitegemea niishije? Niliamua kutokuja hapa ili kuepuka kichaa cha mimba ulichokuwa nacho na bado nimerudi unanichokoza. Chunga mdomo wako Nadina ohooo!. Tena nakwambia usiendelee kunifokea unasikia. Hapa ni kwangu sio kwako umeelewa. Mimi ni mwanaume sipaswi kuulizwa nilipokuwa k**a mtoto. Nadhani umenielewa. Chukua hizi nguo za mtoto, mpumbavu mkubwa wewe. Sura k**a kenge malaya" Herbert alimfokea mkewe kwa hasira huku akiwa anaunyoosha mkono uliokuwa umeshikilia kifurushi kidogo cha nguo kwenda kwa mke wake.

Kwa hasira Nadina alikwapua kifurushi kile kilichokuwa na nguo za mtoto. Kisha akampiga nacho mmewe usoni. Mmewe naye akamsogelea kisha akamrushia kofi zito usawa wa shavuni. Lakini Nadina akaliona akalikwepa. Hebert akiwa amefura kwa hasira akarusha tena kofi jingine lakini safari hii Nadina hakulikwepa isipokuwa alijikinga kofi hilo kwa kutumia mtoto ambaye alikuwa amempakata. Moja kwa moja kofi hilo likatua kwa mtoto na kumfanya aanze kulia kutokana na maumivu aliyoyapata. Hebert naye alipoona kuwa amempiga mtoto ikabidi atulie hakujaribu kurudisha kofi lingine tena.

Hapo sasa mambo yakawa si mambo tena. Nadina akaingia chumbani na kuanza kulia huko pamoja na kichanga chake. Herbert yeye akabaki amesimama hasira zimemjaa. Nadina alilia kwa muda mrefu ila baadae akanyamaza. Mtoto naye akawa amelala hivyo kumpa Nadina nafasi ya kuandaa chakula cha usiku. Mmewe naye moja kwa moja alipita hadi kitandani akalala. Hata mkewe alipokwenda kumuita kuwa chakula tayari alikisusa chakula hicho na kuendelea na usingizi. Nadina alikula kisha naye akaingia kulala. Usiku huo hakuna aliyethubutu kumgusa wala kumuongelesha mwingine.....

ITAENDELEA

Wananchi mnasemaje?
22/07/2023

Wananchi mnasemaje?

20/07/2023

Sipendi wanangu waje wavute bangi! Ndiyo maana napambana kuivuta ili niimalize wakizaliwa wasiikuteπŸ˜₯

ππˆπ‹πˆπŠπ„π’π‡π€_____________Ulinifanya nikeshe, shauri ya utelezi,Nguo safi nijiveshe, yote sababu ya penzi,Kigeto nikisafishe...
07/07/2023

ππˆπ‹πˆπŠπ„π’π‡π€
_____________

Ulinifanya nikeshe, shauri ya utelezi,
Nguo safi nijiveshe, yote sababu ya penzi,
Kigeto nikisafishe, na kumbe kuja huwezi,
Shauri ya utelezi, ulinifanya nikeshe.

Uliiomba nauli, hima hima nikatuma,
Ukasema kwenu mbali, tena miguu yauma,
Safari ya saa mbili, wewe wasema majuma,
Hima hima nikatuma, uliiomba nauli.

Kimbembe ulikianza, ulipotoa mkwanja,
Uongo ukauanza, sasa unapaka wanja,
Safari hujaianza, ila wafuma ujanja,
Ulipotoa mkwanja, kimbembe ulikianza

Kumbe mie maskini, nikashindwa kutambua,
Nkapaka vumbi gogoni, ukija nakukomoa,
Nkasogea mlangoni, kwa nia kukupokea,
Nikashindwa kutambua, kumbe mie maskini.

Yatimu masaa tano, na bado hujatokea,
Simu yako mara tano, na kote hukupokea,
Nkabaki kwenye mabano, ni kipi kimekutokea,
Na bado hujatokea, yatimu masaa tano.

Moyo nikapiga konde, hata usiku sasita,
Usingizi chonde chonde, kulala mwili wasita,
Redio nyimbo za konde, kijiti nikikivuta,
Hata usiku sasita, moyo nikapiga konde.

Sa nane ikatimia, ningali nakungojea,
Vocha kunikatikia, bila simu kupokea,
Arafa kanitumia, eti huwezi tokea,
Ningali nakungojea, sa nane ikatimia.

Nikabaki nikilia, mrungura menilia,
Nguvu zikaniishia, jimbi limejiwikia,
Ashiki zimekolea, kipofu kajinunia,
Mrungura menilia, nikabaki nikilia.

Nitash*taki kwa Mungu, binadamu hakuwezi,
Ili upigwe marungu, wewe tayari ni jizi,
Nayasema kwa uchungu, hutofauti na mwizi,
Binadamu hakuwezi, nitash*taki kwa Mungu.

FAZA HAUSI - 1Kuna wakati bwana maisha yalinichapa kinoma. Yaani nilipitiwa na kiangazi ile mbaya. Sio kwamba sasa hivi ...
26/05/2023

FAZA HAUSI - 1

Kuna wakati bwana maisha yalinichapa kinoma. Yaani nilipitiwa na kiangazi ile mbaya. Sio kwamba sasa hivi niko vizuri!

Hapana, niko vibaya lakini sio k**a kipindi hicho.

Ngoja nikwambie... Kipindi hicho niliishiwa na kila kitu. Mara paaa! unga ukaisha, nikasema nitakuwa napika wali kwa kuwa nilikuwa na kilo kadhaa za chenga za mchele ndani. Nimeuita mchele huo chenga maana ulikuwa na ubora mdogo sana.

Basi bwana, nikawa nikipika ki-boko changu cha wali nakula kwa siku mbili. Mbwa hafi kwa njaa, anauawa na uzee ama ugonjwa tu.

Wakati huo kila nikijaribu kuisaka noti inakosa! Najaribu kuamka asubuhi ili niione hiyo nyota njema ila wapi! Vuja jasho na k**asi, hakuna kitu. Nikijitahidi saana nikavuja jasho na damu naambuli vishilingi hamsini.

Mwishowe mchele nao ukakata! Bahati mbaya iliyoje.

Nikaanza kununua viunga robo napika mara tatu. Mchana napika ugali tonge mbili na uji kidogo. Uji nafanya k**a mboga. mwishowe gesi nayo ikakata.

Majanga.

Hali iliponizidi ujanja nikauza gesi. Saa ngapi mwajuma ndala ndefu hajaimaliza pesa hiyo? Haikumaliza hata siku mbili.

Nikaona liwalo na liwe, nikauza kitanda na godoro lake na mashuka k**a kifungashio. Nilikuwa hata siwazi nitalalia nini. Baadaye niliona isiwe tabu nitalala kwa marafiki.

Nikawa nalala kwa washikaji. mpunga ulipokata tu wakanichoka na kunitimua. Nikarudi geto kwangu nikauza mazaga zaga yangu ya ndani yote. Pesa nikamwagilia moyo.

Hiyo pesa nayo ilipokwisha nikakutana na msala mwingine. Naamka asubuhi na hangover zangu nakutana na Faza hausi akinidai chake. Muda huo sikuwa hata na sh 10 ya kulipa kodi. Halafu muda tayari nilikuwa nikidaiwa miezi mitatu ya nyuma. Ukijumlisha na huo unakuwa mwezi wa nne.

Akili ikagoma kufikiri.

Chimba mkwara mbuzi, faza hausi anaukwepa. Nikaona hataki kuondoka nikamwingizia stori za Simba na Yanga ila wapi hazitaki. Nikagonga mkono na kutetema k**a mayele ili afurahi aondoke, wapi! Yeye akawa amekazania tu pesa yake.

Nikaona ishakuwa nongwa sasa sina cha kufanya.

Mwishowe akaondoka na kuniambia kuwa kufikia jioni niwe nimemlipa la sivyo anatupa vitu vyangu nje. Sasa nikawaza atatupa nini? maana tayari ndani patupuu, ni sakafu yake iliyochakaa tu na manguo yangu.

Aaah! nikaamua k**a mbwai iwe mbwai tu. Tunasikia mbwa kala mbwa ila leo silipi kodi na sitoki hapo mpaka pale tembo atakapomla tembo mwenziye, Eboo!

Jioni hiyooo ikawadia na kigiza chake. nikajiuliza nafanyaje. Nikapata mbinu moja hivi.

Nilikumbuka kuwa mlango wa chumba hicho unafungwa kwa kufuli siyo kitasa. Lakini pia dirisha lake linafunguka na ni kubwa kiasi kwamba mtu anaweza kupita mzima mzima baada ya kulifungua kwa namna fulani ambayo hata mwenye nyumba alikuwa hajui. Nilikuwa najua mimi tu.

Sasa nikaufunga mlango wangu kwa nje kisha funguo nikazitia mfukoni. Nikazunguka na kuingia ndani kwa kupitia dirishani.

Baada ya muda kidogo nikamsikia mwenye nyumba akija maana alikuwa akiishi tofauti na hapo. Nilimtambua kwa tembea yake ya kuburuza miguu chini. K**a kawaida yake nikasikia akijikoholesha. Nikawasikia wapangaji wenzangu wakimpa salamu naye akiziitikia.

Akatembea hadi mlangoni kwangu. Ila kabla hajagonga mlango akaliona kufuli mlangoni. Nikamsikia akisonya na kuanza kufoka. Akawa analishika kufuli.

Akafoka... akafoka... akafoka si kidogo. Akawa anasema akija kesho yake asinikute. Mimi muda huo tuli nimekaa ndani nikichekea mbavuni.

Akafoka mpaka wapangaji wa vyumba vyangu wakajaa mlangoni kwangu wakimpepea na kumsihi apunguze jaziba aende arudi kesho kunitafuta.

Akatulia huku akihema juu juu.

Mara mimi huko ndani nikahisi kiu. Nikanyanyuka ili ninywe maji. Nikakichukua kikombe na kuchota maji ndani ya ndoo moja iliyobaki. Nikayanywa.

Bahati mbaya wakati nakunywa hayo maji si yakanipalia bwana. Nikakohoa kwa nguvu mno na kuwash*tua waliokuwepo nje. Wakahisi labda mimi mchawi maana wanaona mlango umefungiwa nje halafu kikohozi kinatokea ndani.

Muda huohuo tena umeme ukakatika. Eeeh! kuna aliyebaki? wote waliokuwepo walitoka kwa mabio. kila mtu akajifungia chumbani kwake. Faza hausi yeye alitupa mguu mpaka kwake.

Nikajua tayari nimelamba joka, imebakia kumtwanga mtu.

Walipotoweka umeme ukarudi.

Nami nikataka kuitumia hiyo opotyuniti ili niogopwe. Nikapita dirishani nikatoka nje. Nikajifanya k**a sikuwepo. Nikafika kwa kuanza kuchimba mikwara nikiuliza nani alikuwa ananitafuta mida mfupi uliopita. Weeee nakwambia waliogopa mno.

Mbona chakula walinipa wao bila kuwaomba.

Kesho yake simu yangu ikaita. nilipoangalia alikuwa mwenye nyumba. Nilipopokea akaanza kuniomba msamaha. Mwisho wa mazungumzo akaniambia ananiomba niishi hapo bure bilashi kwa mwaka mzima na nikishindwa kupika niwe natoa taarifa mkewe ananileteaπŸ˜„

Mwaka umeisha ila sina hata mpango wa kuhama.

Address

Mwanza

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Riwaya na Hadithi posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Riwaya na Hadithi:

Share

Category