Simulizi za Mude

Simulizi za Mude Huu ni ukurasa wa Simulizi na Makala za kusisimu.

27/11/2022

Hadith:Firimbi.
Mtunzi:Ladislaus Mude.
Sehemu:-8

Makiwa alipofikisha umri wa miaka kumi na moja na wakati huo Mama yake alikuwa tayari ameshafariki, Makiwa alibaki mkiwa hakuwa na furaha tena ya kuishi alitamani kujiua ili apishane na fedhea na manyanyaso ya vijana wenzake.

Akiwa ndani ya usingizi mzito Makiwa atokewa na kitu cha ajabu ajabu upepo si upepo kimbunga si kimbunga kitu hicho cha ajabu kiliongea na Makiwa na kumwambia Makiwa mwana mnyonge wa Chimve, mkombezi na shujaa wa kweli yanini kukata tamaa?, tumekuleta wewe, tumekuchagua wewe ili uiokoe Chimve na watu wake wewe ni uzao wetu ”

Makiwa aduwaaa na kushikwa na uoga moyoni upepo wa ajabu waendelea kusema”usifadhaike moyoni mwako, faraja yako ipo Chimve, itumie vizuri ili ikupe furaha, Aonyeshwa Njiwa akiwa amelalia yai ndani ya pango katikati ya misitu mkubwa na juu ya kilele cha jabari kubwa nje kidogo ya mji wa Chimve.

Makiwa aamshwa usingizini ikiwa ni usiku wa Manani na kuelekea kule alipo onyeshwa na Mizimu, palikuwa ni usiku mkubwa lakini cha ajabu eneo lile palikuwa na mwanga wa ajabu mithili ya theruji ya mlima ulipo nyikani mwa mashariki ya bara giza.

Hakika huwezi kuungalia kwa macho meupe aingia moja kwa moja mpaka pangoni akielekezwa na kipofu jongooo amkuta njiwa mweupee peee akiwa anatamia yai, hakika mbwa hulala chali akimuona bwana wakenjiwa alipo muona Makiwa anaingia alisogea pembeni na kuliacha yai pekeyake.

Makiwa achukua yai lile kitendo cha kulishika tu yai likabadilika na kuwa Firimbi inayo ngaaa, mngao wa dhahabu Makiwa ashtuka toka usingizini na kujikuta akiwa katika msonge wake wa suti mkononi akishika firimbi ya yake.

Firimbi ilikuwa na maajabu mengi kwanza hupigwa na mtu mmoja pili hupigwa kwa kutumia tundu za pua wakati wa shida maalum au panapo hitajika msaada wa jambo fulani sio mdomo, kipindi inatoa sauti basi maadui wote upatwa na usingizi mzito pia hutoa sauti inayo burudisha, kuliwaza na kukupa tumaini, firimbi hiyo ya ajabu huja kipindi cha tukio tu na hubadirika kutokana na matukio na sehemu.

Makiwa aingiwa na uoga na hakuamini alichonacho mkononi kwani alijua ni ndoto tu aliamua kuendelea na utamaduni wake wa kuimba na kupiga firimbi, watu wengi walimdharau na kumuona ni mtu fukara na ombaomba vijana wenzake walimtenga kisa alizaliwa na wazee na wengine kumuita mtoto wa ajuza wengine kumuita mtoto wa mkorechi.

Mizimu ya Chimve ilimpenda Makiwa kwani ndio lililozao lao la pekee nje ya ukoo wa Chifu na walimlinda kwa kila janga walifanya kila liwezekanalo Makiwa aishi ingawa hawakuweza kumpata akili ya utambuzi juu ya matumizi ya firimbi yake ya ajabu.
UGENI WA MGENI.

Siku zimepita mgeni azoea Chimve watu walizidi kumshangaa mgeni washindwa elewa nani kaja nini kafata, mgeni alikuwa ni mtu tofauti na watu wa Chimve kitabia na kimuonekano watu wengi walihisi ni miujiza ya Mizimu kuleta kiumbe kile ingawa kilikuwa kinaongea na kuandika.

Rangi ya mwili wake nik**a tunda la mpapai, mwili wake una vinyweleo k**a ngozi ya kondoo nywele zake laini k**a nyuzi za fusi macho makali yenye kumetameta k**a vito vya kuta wa mji wa Chimve, hekima yake ipo juu mithili ya ndege njiwa, kinywa chake kitamu k**a ndege kasuku sura yake ya upole k**a nyani mtegoni hakika wana Chimve walistaajabu kumuona kiumbe kile.

Kutokana na utofauti wake Wana-Chimve walimpeleka mpaka kwa Chifu wao Chemvue, Chemvue alimkaribisha na kumpa kibuyu cha ugimbi k**a ishara ya ukaribisho na kumfanya awe huru na Amani Chemvue alimuhoji yeye ni nani amekuja kufanya nini.ingawa lugha iliyotumika ni ishara na michoro tu.

Itaendelea............

03/11/2022

Hadithi:-Firimbi.
Sehemu:- 7.
Mtunzi:-Ladislaus S Mude.

Wale askari walipofika kwa Mbonane na walimpa taarifa ya Chifu wao, huku mjini Chimve Mganga mkuu tayari alishaona na kujua lilipo moyoni mwa mvamizi hivyo alimwambia bwana wake juu ya kujipanga kivita na mtu jasiri mwenye akili na mbinu kemkem za kivita.

Chifu Gwindwa alijiandaa vizuri na kuwaweka askari wake utimamu wa akili na mwili alimwita Baba-Makiwa afanye kazi yake ya kuwaliwaza askari wake kwa nyimbo za kishujaaa na ngoma za kuhamasisha walienda juu ya kilele cha mlima mrefu kuliko wote katika bara giza.

Mlima wenye theluji nyeupe na hali ya hewa ya ubaridi mkubwa ilikuweka miili yao sawa mlima uliozungukwa na msitu mkubwa na wanyama wa kila aina bila kusahau ndege wa rangi mbali mbali, hakika walipata tulizo la kweli mlima huo wana Chimve waliuita kilimankyaro yaani kilicho chetu.

Mbonane aliwau askari wawili na kumuacha mmoja ili aende kutoa taarifa kwa bwana wake, kutokana kwa kitendo cha Chifu kupeleka ujumbe wa maongezi ya Amani Mvamizi Mbonane aliona kuwa ameogopeka na Chifu Gwindwa ni dhaifu hivyo angeweza kushinda vita hiyo.

Mbonane anajindaaa kuvamia Chimve Chifu wa Chimve achukua jeshi lake na kuliweka sawa ili kujilinda na mvamizi wake jeshi la jenga lashuka toka mlima na kuelekea mipakani wakiwa na mkuu wao Gwindwa, huku kukisikika ngoma na nyimbo za kuhamisisha na kutia moyo.

Siku imefika kazi imeanza Mbonane Matabane uwanjani Gwindwa Chimve Chengula kazini hakika hapakaliki wa hapasimamiki mapigano ya mbinu nyingi kutoka kila upande askari wengi walipotea kutoka kila pande, Mbonane mara nyingi utumia mbinu ya nyuki Malaika kati Gwindwa aliamua kutumia mbinu ya mbwa mwitu na siafu kushambulia.

Walishambulia kwa mfululizo bila kusimama kwa ushirikiano mkubwa hapo ndipo tulipoana uhodari wa jeshi la jenga katika kutupa mishale, Baba-Makiwa alichukua mzinga wake na upinde na kuanza kazi ya kurusha mishale kwa aina ya mwendo nyoka maji, Baba-Makiwa alikuwa na uwezo wa kurusha mishale minne kwenye upinde mmoja yote utoka kwa aina ya konakona.

Jeshi la jenga lilikuwa linaanza kuelemewa kutoka kwa wavamizi uhodari wa Baba-Makiwa katika matumizi mazuri ya mishale kwa mtindo wa mwendo wa nyoka maji ndio uliyo warudisha mapambanoni Mbonane na jeshi lake walishindwa kudhibiti kimbunga cha mishale toka kwa Baba-Makiwa.

Wapiga ngoma nao hawakusimama kupiga na kuweka molari kwa askari wao kila mdundo uliendana na mishale mia moja, wavamizi walipigwa bila uhuruma walisogezwa mpaka kilima hewa Mbonane alishindwa vita na kukimbia.

Miezi ilipita na mtoto kuzaliwa hatimaye Mama-Makiwa ampata mtoto wa kiume na kumuita jina Makiwa yaani mwana mnyonge huzuni mahala pake Makiwa na mama yake waliishi maisha ya kifukara katika kijumba kidogo cha msonge wa suti, Makiwa akiwa katika umri wa miaka 7 alikuwa anapenda kupiga firimbi huku akiwa anaimba barabarani k**a njia ya kujipatia kipato ili aweze kumsaidia mama yake ambaye ni mzee Maisha yaliendelea hivyo.

Itaendeleaa........

28/10/2022

Hadithi:-Firimbi.
Sehemu:- 6.
Mtunzi:- Ladislaus S.Mude.

Baba-Makiwa akiwa na babu yake waliwasili msituni hapo muda wa usiku wa Manani kukiwa na giza nene la usingizi wa pono, Babu alianza kuomba Mizimu kwa kutumia lugha ya kimizimu huku kukivuma upepo mkali unao ongea lugha hiyo, wakiwa wamejimwagia damu ya kondoo mchanga mwenye rangi nyeupe asiye kuwa na doa lolote mwilini mwake.

Upepo uliendelea kusema na kuvuma mvumo wa ajabu na wakutisha majani na miamba yote ikiwa imetulia ishara ya kutii na kuheshimu Mizimu babu akiendelea kuomba ili mjukuu wake abarikiwe na kukubaliwa kukabidhiwa firimbi hiyo.

Kazi haikuwa rahisi Babu alijitolea juu ya mjukuu wake kwa sharti la kutoa kafara ya damu yenye chumvichumvi, kwa mapenzi yake juu ya mjukuu wake wa pekee na kipenzi chake Babu alikubari kujitoa kafara ili azma yake hitimie.

Babu Amgeukia mjukuu akiwa na paji la huzuni usoni, chozi la dondoka ardhini, tabasamu kinywani, mjukuu kiza chatanda, hajui hata parapanda, busu la agano utosini, firimbi ya ajabu mkononi, babu atoweka kimbungani.hiyo ndio ilikuwa siku ya Baba-Makiwa kukabidhiwa firimbi hiyo hakika Mizimu ilivutiwa na ukarimu, hekima na busara ya Baba-Makiwa.

Baba-Makiwa alipelekwa mpaka katika uwanja wa mzoezi wa jeshi la jenga na kusajiliwa k**a askari wa jeshi hilo akiwa kijana wa makamu, walianza mafunzo mara moja Baba-Makiwa alikuwa ni mtu mwenye haiba ya aibu na asiye penda kudharauliwa ingawa alikuwa na uwezo mkubwa wa kurusha mishale na kupiga firimbi kwa ustadi mkubwa.

Wakiwa katika mazoezi ya kijeshi Baba-Makiwa alipewa kazi ya kuburudisha askari wenzie kipindi wakiwa vitani, aliifanya kazi hiyo kwa ustadi na uweledi mkubwa Siku moja wakiwa uwanja wa vita jeshi la jenga lilivamiwa na majeshi kutoka kusini ya mwisho mwa bara giza watu hao walitambulika k**a Mgongoma, jeshi hili lilikuwa lina ongozwa na mtu mmoja aitwaye Mbonane Matabane.

Mbonane alikuwa ni shujaa wa vita aliyeshindikana lakini jeshi la jenga lilifanya kazi kubwa kumdhibiti kiumbe hiki, mji wa Chimve ndio mji mkuu kwa taaluma ya kufua vyuma na utengenezaji wa silaha, walipata elimu hii kupitia babu zao katika jando na kuhifadhi kwa maandiko ya michoro mapangoni.

Wana Chimve walikuwa wanapenda kujifunza na kufunza watu wao juu ya maisha ya kujitambua na kujilinda, walitumia mila ya jando na unyango kutoa mafunzo hayo, kwa kuwa walikuwa bado hajangundua njia rahisi ya utoaji elimu k**a maandishi ya herufi na silabi.

Wao walitumia k**a njia ya kufundishia mfano ngoma, uchoraji kwa kutumia mawe, kuiga kwa kuona ufumaji, ususi na uhunzi au ufuaji Kwa kupita elimu hii wana Chimve walikuwa hodari kwa kufinyanga vyungu vya kuwekea maji wakiwa vitani na silaha imara na nyepesi kutumia ngao zao zilikuwa ni madhubuti mno, mavazi yao ni Zaidi ya ngao.

Walikuwa ni watu wa mtazamo tofauti na jamii nyingine wastaharabu, wanao jitambua wasiopenda kuonewa wala kutawaliwa kimabavu, waliishi kwa umoja na upendo mkubwa waliheshimiana kwa kila rika maisha yao yalikuwa ni k**a pepo ya mungu kwa Amani na furaha.

Mbonane alipofika mpakani mwa mji wa Chimve Chifu Gwindwa aliwatuma askari wake waende kwa Mbonane ili aweze kufanya nae maongezi ya Amani, Mbonane alikuwa anatafuta sehemu ya kuweka ngome yake alikuwa k**a kipofu alipapenda Chimve kutokana na mali na mazingira mazuri ya mji wa Chimve na vivutio mbali mbali k**a milima, maziwa na mito.

Hakika firimbi ilikuwa na maajabu, Baba-Makiwa aliitumia firimbi k**a silaha ya kuwindia wanyama hupiga na kumfanya mnyama kusudio kulala chini k**a mwenye kusubiria kuchinjwa, pia aliitumia k**a taa penye giza ustadi wake wa kupiga Firimbi ulimfanya Mama-Makiwa kupata tulizo la moyo na faraja ya nafsi hasa kipindi cha usiku wakiwa wameketi wa kiota moto.

Mama-Makiwa naye hakuwa nyuma alimsindikiza mumewe kwa kuimba nyimbo ya tumaini lao la maisha Rabana alimpa sauti nzuri na yenye mvuto mithili ya Bi Shakira Said wa JKT Taarabu, familia hii hakika ilikuwa imejaa vipaji lukuki kwenye uwimbaji na upigaji wa ara za mziki.

Siku hiyo akiwa katika mawindo yake alimuona nyoka mkubwa mwenye rangi mchanganyiko alipiga firimbi yake k**a kawaida na alifanikiwa kumk**ata nyoka yule lakini siku yake ilikuwa imeshafika ya kafara kufanyika nyoka alimgonga Baba-Makiwa kidoleni, Nyoka alifanikiwa kutoweka palepale pasipo kujulikana alipoelekea Baba-Makiwa alirudi nyumbani kuuguza kidonda chake kilichodumu masaa matatu tu kabla ya kupoteza uhai wake.

Itaendelea..........

20/10/2022

Hadithi:-Firimbi.
Sehemu = 5.
Mtunzi:- Ladislaus S. Mude.

SAFARI YA CHIFU CHEMVUE.

Chemvue anza safari na askari wake kuelekea Nyamirembe wakiwa njiani walipambana na majeshi mbalimbali ya watekaji waliokuwa na lengo la kunyanganya silaha na mali zao lakini kwa utayari wao Chemvue na jeshi lake hasa ukizingatia walitoka katika mapambano makubwa waliweza kushinda na kufanikiwa kusonga mbele.

Waingia Nyamirembe muda wa jioni kukiwa kunakaribia machweo wafika malangoni mwa mji wa Nyamirembe, Chemvue hakuamini anachokiona mbele ya malango ya mji wake alioutolea jasho na kusababisha kifo cha shujaa wake wa pekee.

Chifu Gwindwa alishatuma askari wanne wenye nguvu za kichawi na mbinu kali za kivita kuulinda mji ule kwani ni mali Chimve.

Chemvue aishiwa nguvu na mawasiliano ya miguu na ubongo vyashindwa kwenda sambamba ajikuta ameketi chini kwa kushindwa kuingia mji ule ambao aliutolea jasho, aamuru askari wake warudi mpaka mlima Chengula na kuweka kambi pale ili walale mpaka kesho asubuhi ndio waangalie wapi waeleke.

Muda wa utawala wa mwezi na nyota ulipo simamisha usinga wake Fundi chuma alinyanyua vilango vyake na kuwatoroka askari wake na kuelekea upande wa magharibi akiwa peke yake achukua silaha na kibuyu cha asali jasiri asahau asili.

Ndani ya mji wa Chimve palikuwepa watu wawili walioishi miaka mingi bila kupata mtoto ujanani mwao watu hao walijulikana kwa jina la Baba na Mama-Makiwa hii ni kutokana na hali yao ya upweke na majonzi kwa muda mwingi, familia zingine za rika zao na walio wazidi rika katika ndoa wana watoto na wengine wajukuu na vitukuu lakini wao Mungu hakuwabariki kupata mtoto.

Siku moja mji wa Chimve walipokea mgeni ambaye walishindwa kujua wapi ametokea ila kutokana na mji huu kuwa ni mji mashuhuri wa kibiashara hawakuwa na shaka nae maisha yaliendelea k**a kawaida na mgeni alijumuika kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ndani ya jamii ya Chimve.

Mama-Makiwa mara nyingi huenda kuomba Mizimu ili iweze kumpa mtoto japo mmoja wazee hao walipofikia umri wa miaka 50 ndio Mama-Makiwa akafanikiwa kupata ujauzito, aikumchua mda mrefu Baba-Makiwa kufariki kwa kugongwa na nyoka mkubwa kidoleni kutokana na masharti ya Mizimu.

Mizimu ilitoa sharti la kafara ya damu ya chumvi itolewe Baba na Mama-Makiwa walikubaliana kwa hilo ila palikuwa na fumbo ndani yake juu ya nani na lini kafara hiyo itafanyika hakika hili ni fumbo la imani.

Baba-Makiwa alikuwa na uwezo mkubwa wa kuchezea na kuk**ata nyoka utumia firimbi katika shughuli zake za kuk**ata nyoka na alirithi uwezo huo kutoka kwa mababu zake ingawa alikuwa ni mtu mwenye uwezo mzuri wa kurusha mishale tena umbali mrefu.

Mafunzo haya aliyapata kutoka kwa babu yake mzaa mama ambaye alikuwa ni mtu mwenye kulenga vizuri shabaha kwa mtindo wa mwendo nyoka, Baba-Makiwa alipata mafunzo hayo kupitia jando la kishujaa pembezoni mwa Mji wa Chimve Baba-Makiwa akiwa katika shughuli zake za kuwinda mara akutana na askari wa Chifu Gwindwa wakiwa wanakusanya watu kwa ajiili ya kuujenga mji wao.

Baba-Makiwa akiwa kijana mdogo aliongozana na babu yake mzaa babaye kwenda katika msitu mkubwa wenye majabari na miamba mikubwa huko ndio Baba-Makiwa alipo kabidhiwa filimbi yenye maajabu ya kustaajabisha.

ITAENDELEA........

13/10/2022

Hadithi:- FIRIMBI.

Sehemu:- 4

Mtunzi:- Ladislaus S Mude.

Chemvue na baadhi wa askari wa kiwa njiani kuelekea mjini Chimve wakiwa na mwili wa marehemu Chengula waliendelea kuimba nyimbo zao za kishujaaa zikiambatana na milio ya silaha zao kwa kuzingonganisha, hakika walipata taabu njiani kwani kulikuwa na misukosuko mengi ukiacha mvua, upepo mkali na miungurumo ya baragumu.

Walikuwa wakipambana na wanyama wa kali ila cha ajabu kipindi wakiwa katika mapambano hayo kundi kubwa la nyuki linakuja kuzunguka mwili wa Chengula k**a ishara ya ulinzi juu yake na kutengeneza asali na nta iliyo bora kwa ulinzi wa mwili wa Chengula amakweli “zimwi likujualo halikuli likakwisha Mizimu iliendelea kumlinda Chengula ili afike salama katika ardhi ya ma-babu zake.

Chemvue aingia Chimve akiwa na askari mia tano na kenda huku wakiwa wameubeba mwili wa Chengula walipo kanyaga ardhi ya Chimve tu na giza lilitoweka palepale na mvua ndogo ilinyesha k**a ishara ya ukaribisho wa Chengula katika ardhi ya asili yake hakika Mizimu ilimpenda Chengula kutokana na upendo wake kwa jamii yake ingawa Wana-Chimve hawakulijua hilo kutokana na upofu wa jongoo aliyowafanyia Chengula kwa kujifanya mlevi wa kutupa na asiye kuwa na maadili mema hakika usipokijua kivuli chako, hutojua nyendo zake.

Chifu Gwindwa na mkewe wakiwa malangoni ya ki-Chifu wakisubiria kuupokea mwili wa kifungua mimba chao Chengula au mtoa ujana wao waliuchukua mwili ule na kuupeleka sehemu ya kuifadhia huku wakiendelea na utaratibu wa mazishi Chemvue baada ya kuukabdhi mwili kwa wazazi wake alielekea kwenye boma lake na kujilaza machozi yalishindwa kusimamisha mwendokasi wake.

Chengula ni mtoto wa kwanza wa Chifu hivyo atazikwa kwa heshima zote za kijadi za uzao wa kwanza wa kichifu, k**a kuupaka mwili wake mafuta ya asali ya nyuki wadogo waliojenga mzinga wao kichuguuni na kumuwekea sarafu ya kweme machoni mwake, kumvesha mavazi ya kivita yakiambatana na silaha yake.

Siku ya mazishi imefika palipikwa pombe nyingi na kuchinjwa kondoo kumi wa uzao wakwanza ili kusindikiza mazishi ya jasiri wa vita Chengula kipenzi cha wanafamilia ya kichifu na Juata msichana mrembo wa Katoro na kutimiza maagizo ya Mizimu na mila za Wana-Chimve.

Ndani ya shimo kulimwagwa damu ya kondoo na kutandaza ngozi ya kondoo, wakaulaza mwili wa Chengula juu yake waliufukia mwili wa Chengula na kumwagia pombe mazishi yaliishia hapo na ndipo palikuwa nyumba yake ya milele Jasiri wa Vita Chengula Gwindwa Chimve.

Waliomboleza kwa mda wa siku saba kwani ndio utaratibu wao hasa kwa mtoto wa kwanza wa kiongozi yaani Chifu baada ya maombolezo kuisha Chifu Gwindwa na viongozi wengine walikaa kikao juu ya Chemvue kwa kitendo cha kutoroka na jeshi la jenga na kupelekea kifo cha mrithi wa Chifu.

Kikao kiliendelea kwa siku tatu mfululizo huku baadhi ya viongozi wakishinikiza kuwa Chemvue ahukumiwe kifo na wengine afukuzwe ila maamuzi yote yapo chini ya Chifu Gwindwa, Chemvue barazani mbele ya wazee wa ukoo Baba mzazi wa Chemvue hatimaye anatoa hadhabu na Chemvue afukuzwa Chimve na kukabidhiwa silaha na askari baadhi wa jeshi la jenga.

Chemvue ndie mtu pekee ajuaye uzao wa kaka yake Chemvue aondoka Chimve kuelekea Nyamirembe katika mlima Chengula huku akiwa na kumbukumbu ya kifo cha kipenzi chake rafiki yake na mwalimu wake mkuu wa upambanaji jasiri wa vita Chengula Gwindwa Chimve.

ITAENDELEA..............

Hadithi:- Firimbi.Mtunzi:-Ladislaus Mude.Mara Chengula akata kauli, afumba macho, mapigo ya moyo yasimamisha mwendo na k...
06/10/2022

Hadithi:- Firimbi.
Mtunzi:-Ladislaus Mude.

Mara Chengula akata kauli, afumba macho, mapigo ya moyo yasimamisha mwendo na kushindwa tembea tena na huo ndio ulikuwa mwisho wake, ama kweli nyota hupoteza nuru baada ya kucha Chengula aaga dunia mikononi mwa Chemvue.

Chemvue alipiga yowe kubwa huku akimtikisa kaka yake lakini aikusaidia kitu kwani kibuyu cha mtindi kilisha pasuka na samri kupotea, askari mmoja alifuata Chemvue na kumnyau pale kisha kumweka pembeni, waliuchukua mwili wa Chengula na kuweka sehemu salama na kuupaka majani ambayo usaidia mwili kutoharibika.

Chemvue aliamuru baadhi ya askari wabaki pale Nyamirembe na ile sehemu aliyofariki kaka yake alipaita Chengula (mlima Chengula) alfajiri ilipofika walianza safari kurudi kwao Chimve.

Walikuwa wanaimba nyimbo za kivita za kuleta matumaini na kufarijiana wenyewe kwa wenyewe iliwachukua muda wa siku kumi na nne njiani huku wakipatwa na misukosuko ya mvua kubwa na upepo mkali ikiwa ni ishara ya Mizimu ya ukoo wa kichifu kukasirishwa na kitendo cha watoto wa Chifu kutoroka na kusababisha damu yao kutiririka katika ardhi ya ugenini pasipo na Baraka za Mizimu hiyo.

Mjini Chimve palikuwa na wingu kubwa na giza nene lililo ambatana na ukunguu mkubwa wa hapa sitoki, kule sioni kwa siku kumi na nne na masaa matano.Chifu Gwindwa na waganga wake walijua kilichotokea kwani ndio utaratibu wao k**a Mizimu ikikasirika huwa kuna kuwa hivyo au kunanyesha mvua kubwa na maafa hutokea.

Chengula alipo jeruhiwa Mizimu ilituma salamu kwa mganga mkuu wa Chimve kwa njia ya ndoto na kumpa taarifa zote juu ya majeraha ya Chengula na hitimisho lake, Hakika mganga alishtuka kupata taarifa hiyo.

Wana-Chimve walikuwa na tashwishi miyoyoni mwao kwani hawajui usiku ni upi au mchana ni upi muda wote ni giza tena giza nene la ajabu waganga walijitahidi kuomba radhi kwa Mizimu hiyo na hawakujua kosa walilo fanya mpaka kupelekea adhabu tarajiwa ingawa mganga mkuu alishatambua hilo.

Mizimu haikuishia hapo katika kusambaza taarifa za kifo za mtoto wa uzao wa kwanza wa Chifu mara hii taarifa ilienda moja kwa moja kwa mama mzaa chema.

Mke wa Chifu Gwindwa alioteshwa kuwa kuna maji ya damu yakitiririka kuja katika mji wao mara akamuona mwanae Chengula akiwa anaelea juu ya maji k**a vile mtu aliyekufa akashtuka kwa kupiga ukunga mkubwa, Chifu Gwindwa alimuulizanini tena mke wangu mpenzi mbona wapiga yowe hivyo? mke wa Chifu alibaki analia tu alishindwa kuongea kwa muda.

Ndipo Chifu aliamuru waganga waje na waelekee chumba cha mkutano yeye akiwa ndani na mkewe alimuuliza tenamama mzaa utawala nini umekiona? mke waChifu alimuangalia mumewe na kuanza kulia, mke wa Chifunimemuona Chengula kipenzi chetu jamaaaniii Chengula wanguuu
Chifu umemuona wapi tena na anafanya nini?
Mke wa Chifu akiwa analia huku akitoa sauti ikiambatana na kwikwi maamaaji ya daddaamuu majiiiiiiiiii mume wanguu yanakukukuuujaaaaaaa.

Chifu anashindwa kuelewa “maji ya damu yanakuja, yanakuja wapi? na Chengula amefanyanini, ebu shusha pumzi mjangaua wangu Chifu akamlaza mkewe mapajani mwake huku akimshikashika kilemba chake na kumfuta machozi.

Mke wa Chifu apata faraja toka kwa mumewe na kuanza kuelezea ndoto yakenimeona maji mengi yanakuja toka milimani, maji ya damu yakiwa na mwili wa mwanetu kipenzi, simba wa vita na mrithi wako wa baadae Chengula”

Chifu alishtuka aliposikia taarifa ya ndoto ile, moja kwa moja alienda kwenye chumba cha mkutano na kuwa kuta waganga wake wameshakaa wakimsubiri.aliketi kwenye kiti chake na kuanza kuwaelezea juu ya ndoto ya mkewe.

Wanganga waliisikiliza vizuri ile ndoto na kuanza kuichambua kwa kuangalia tukio la Giza nene na ukungu wa ajabu ambao bado unawasumbua na kulinganisha na tendo walilolifanya watoto wa Chifu wao kwa kutoroka na jeshi la jenga.

Waganga waliomba mda kwa mkuu wao ili waweze kuangalia na kumpa majibu yaliyo sahihi ili wachukua dakika kumi tu kutoa majibu, Mganga mkuu kutokana na miiko ya Mizimu yetu na kitendo cha watoto wako kukiuka miiko hiyo Mizimu ilikasirika, huko waliko Chengula ameshakufa na wapo njia wanakuja na ndio maana Giza hili lipo na litaisha siku watakayo fika.

Mizimu imekasirishwa kwa Chengula kufa kwenye ardhi ugenini na kosa hilo amelifanya Chemvue kwa kuamuru atolewe kipande cha mshale kifuani, Mizimu bado ipo karibu nao kwa kuwalinda na maadui wote wanao wajongea karibu yao, mwili wa Chengula upo salama na boda damu yake ni mbichi k**a mtu aliyefariki mda huu.

Chifu Gwindwa alinyanyuka pale na kuelekea chumbani kwake na kumuelezea mkewe yote aliyoambiwa na waganga wake, Wasaidizi waChifu walipiga la mgambo nakutangaza taarifa za kifo cha mtoto wa kwanza wa Chifu (Chengula).

ITAENDELEA............

Hadithi:- FirimbiMtunzi:- Ladislaus Mude.Ndani ya uwanja wa vita kati ya jeshi la Jenga na Himaya ya Nyamirembe,Je jeshi...
29/09/2022

Hadithi:- Firimbi
Mtunzi:- Ladislaus Mude.

Ndani ya uwanja wa vita kati ya jeshi la Jenga na Himaya ya Nyamirembe,Je jeshi la jenga chini ya Chemvue litaweza kufua dafu? Hilo ndilo swala pia maisha ya watoto wa Chifu Ngwindwa yatakuwaje?.

Tuendelee

Siku ya tatu Chemvue (fundi chuma) na jeshi lake waingia tena uwanja wa vita, Wakiwa katika uwanja wa damu (mapambano) kaka yake na Chemvue anayefahamika kwa jina Chengula alipigwa mshale upande wa kushoto wa kifua chake.

Chengula alikuwa ni mtu jasiri aliukata mshale ule na kukiacha kipande palepale kifuani na kuendelea na mapambano Chengula akiwa uwanja wa vita daima mwili na akili yake huwa ishajitolea kufa kwa lengo la kupata ushindi tu na daima hakati tamaa.

Chengula alikuwa shupavu na mwenye kujari jamii yake ingawa alikuwa mlevi na mpenda wanawake, ila kila Njiwa na Malaika wake Chengula alizama katika penzi zito la binti mmoja mpika mkomboti wa Katoro.

Mapambano yalikuwa makubwa yalidumu kwa muda wa masaa kumi na robo bila kusimama, hatimaye jeshi la jenga lafanikiwa kupata ushindi kwa kumuua Chifu wa Nyamirembe na kuiweka Nyamirembe chini ya himaya yao.

kwa sasa walipoteza askari wasio pungua mia tano mji wa Nyamirembe ulikuwa una nuka damu na moshi, huku kukiwa na madimbwi ya damu na machozi ya watu waliopoteza wapenzi wao hakika vita sio sherehe wala ngoma ya unyago.

Chemvue pasipo kujua kuwa kaka yake amejeruhiwa aanza kumtafuta kila sehemu bila mafanikio Chemvue anachanganyikiwa kwani anampenda nduguye askari mmoja amuona Chengula akitokwa damu nyingi kifuani, upanga mkononi ukiwa unatiririka damu mithili ya maporomoko ya maji toka mlimani.

Askari alimfuata Chengula kwa ukaribu ndipo aligundua kuwa kiongozi wake ana tatizo katika mwili kwani alianza kuishiwa nguvu alimsaidia kwa kumbeba na kumpeleka kwenye boma lao.

Chemvue afika bomani na kumkuta kaka yake akiwa hoi na hajitambui aliamuru madaktari wamtibie haraka, walianza kwa kumfuta damu zilizokuwa zimetapakaa mwilini mwake na walimtanua mdomo na kumwekea mjiti ili wakiwa katika harakati za kumtoa mshale asiweze kungata ulimi.

Walifanikiwa kumtoa kipande cha mshale na damu iliruka juu mara moja k**a mshale wa kikaguru kisha ikaanza kutiririka k**a maji mferejini Chengula alishtuka kwa uchungu kwa kipande cha mshale kilicho toka na nyama ya kifua.

Chengula alifungua macho na kumuona mdogo wake akamuita kwa ishara kwani hakuweza kutoa sauti kubwa Chemvue amsongelea kakaye, Chengula amwambia nduguye najua unaumia ila jua wewe ndie mkuu wa Chimve mlinde mama na nduguzo pia nakukabidhi mwana wako yupo kwa Yule binti ninapopenda kunywa ugimbiwalicheka kwa pamoja kisha Chengula akaendelea.

Chengula mwisho wangu ndio huu na kibuyu changu kimeshakuwa na nyufa daima nitakuwa nawe sitakuacha nakupenda mdogo wangu, damu yangu haimwagiki bure hapa ni kwako sasa na kukabidhi kwa mikono yangu yenye damu ya kishujaa na ujasiri”.

Chemvue amjibu kakaye huku wakitokwa na machozi hapa ni kwetu usiniache mwenyewe kaka usiondokee, baba na wadogo zako tunakuhitaji mwana wako anakuhitaji bado, wajua mimi ni fundi mzuri wakufinyanga na kuchonga nitakitengeneza tu kibuyu kaka si wajua jina langu mimi ndio fundi chuma”
Chengula amuangalia nduguye huku akitokwa na machozi ashindwa kujibu.

Chengula ananyanyua kinywa chake na kumuagiza nduguye aende kwenye mlima uliyo jitenga mwisho wa Katoro uliyopo upande wa matua jua kuna kichaka kidogo ambacho ndani yake kuna makazi huko ndipo kwenye kweli kweli yake.

Je nini maana ya maagizo hayo, Maisha ya Chengula yatakuwaje?.

Usikose wiki ijayo.

Inaendelea.

22/09/2022

hakuna kidole kilicho muhimu zaidi ya kingine ingawa havilingani umbo wala kimo

22/09/2022

Hadithi-: FIRIMBI.

Mtunzi:-Ladislaus S Mude.

Simu:- 0717929304

Mnamo miaka ya 1899 katika nyika ya unyikani ya mashariki mwa Afrika palikuwepo na Mji huitwao Chimve, Mji wa Chimve ulikuwa unaongozwa na Chifu mwenye nguvu, busara na mwenye kupenda watu wake, Chifu huyo kwa jina Chemvue almarufu fundi chuma.

Chifu Chemvue alikuwa ni mtu anayependa kuwinda na kupigana vita vya mara kwa mara, alikuwa na nguvu, mbinu za kivita na jeshi imara alifanikiwa kila avamiapo hata majirani zake walimuogopa na kumuheshimu walimpachika jina la ndege fundi chuma kwa uhodari wake wa kujenga ngome imara na kuvamia.

Katika mji wa Chimve palikuwa na utaratibu wao wa kiutawala kabla ujakabidhiwa mikoba ya uchifu ni lazima uwe umeshinda vita tatu kwa kuvamia na kulinda, umri usiopungua miaka kumi na tano na kushiriki jando la kishujaa na mashujaa waliopita.

Wana Chimve uishi kwa sheria za kichifu unapokutwa na kosa la kuua, kubaka au kutembea na mume au mke wa mtu basi unyongwa hadharani, wizi, uchochezi na uzembe kazini makosa hayo adhabu chini ya Chifu atakacho amua, familia ya Chifu pekee ndio inayo weza fanya mambo juu ya sheria kwani mali zote ni mali za Chifu hata miili yao pia.

Wana-Chimve walikuwa wanashughulika na shughuli mbalimbali k**a ukulima, uwindaji, ufinyanzi, uchimbaji wa vito vya thamani, ususi na uhunzi wa vifaa vya kulimia na silaha, hivyo Mji wa Chimve ulikuwa ni mji mashuhuri kwa biashara mbalimbali na wageni walikuwa wengi wa kuingia na kutoka.

Kifupi ulikuwa mji mkuu wa kibiashara, biashara mbalimbali zilifanyika zikiwepo silaha, vifaa vya kulimia na vitambaa vya silaa pia vito vya thamani ingawa walikuwa hawana elimu nzuri juu ya uthamani wa vito hivyo.

Mji huu umezungukwa na milima mirefu na misitu mikubwa ambayo uwafanya maadui kushindwa Kuvamia mara kwa mara wana-mji huu hutegemea maji yao kutokea milimani na miamba ya milima kwa ujenzi wa ngome yao na kuchimba vito vya thamani.

Misitu inawasaidia kwa kuchuna nyuzi kwa ajiili ya kufumia vitambaa na kamba pia magome ya miti na mizizi utumia kwa tiba na lishe kwa wajawazito na wazazi hakika ngome ya Chimve ni zaidi ya chuma cha pua kwa uimara wake.

KUFUKUZWA KWA CHEMVUE.

Chemvue (fundi chuma) ni mtoto wa pili wa Chifu Gwindwa, Chemvue alikuwa na kaka yake mkubwa na dada zake wawili walio changia baba Chemvue alizaliwa pekee yake kwa uzao wa mama yake ambaye alikuwa ni mke mdogo wa Chifu Gwindwa, kaka yake na Chemvue alikuwa ni mtu anayependa ulevi na wanawake ingawa ni mwindaji na mpiganaji mzuri katika uwanja wa mapambano asiye kata tamaa, Baba yao aliwapenda watoto wake wote wa nne.

Akiwa katika umri wa miaka kumi na nane Chemvue na kaka yake walienda kuvamia mji wa jirani pasipo idhini ya Baba yao walichukua askari takribani elfu moja mia tano na kenda.

Walitembea umbali wa siku kumi na moja na nusu kufika katika Mji wa maadui (Nyamirembe) walisimika maboma yao umbali wa kilomita kumi toka kambi ya maadui, Chemvue ndie aliyekuwa mkuu wa msafara huo kwani alikuwa ana mbinu nzuri za kivita ingawa alikuwa mdogo kuliko wote kiumri.

Chemvue aliwatuma wapelelezi wake kwenda kuangalia ngome ya maadui ili waweze tambua njia na mbinu za maadui, hakika wapelelezi wa Chimve wanajua wanachokifanya walifanya kazi yao kwa uweledi mkubwa na kwa muda mfupi , walipenya k**a ngoswe mpaka ndani ya mzinga pasipo nyuki kujua kinachoendelea.

Walikaa nao kwa muda wa siku nne wakiwa k**a wageni wa kutoa burudani masokoni, barabarani na kumbi za starehee za maadui, watu wa mji huu waliwapenda kwa muda mfupi pasipo kujua wanakumbatia upupu kwa mikono yao wenyewe.

Wakiwa katikati ya shughuli yao walifanikiwa kujua wapi maadui wana weka silaha zao na idadi yake, maghala ya vyakula na maficho makuu ya Chifu na makao makuu ya askari leo ndio nimeamini msemo usemaousimdhalau usiyemjuaWana-Nyamirembe waliwachukulia k**a mahayawani wasio jua waendako.

Wakina Chemvue walisimika maboma yao katikati msitu huku akiwatuma walinzi wake wakae juu ya vilele vya milima ili kujua wanao kuja na wanaelekea upande gani kwa mgawanyo huu wa kazi ni zaidi ya nyuki mzingani au mchwa kichuguni.

Baada ya wapelelezi wake kurudi akiwemo kaka yake na Chemvue walikaa kikao kifupi cha kupanga mashambulizi jua lilipo zama na mwezi kuchomoza Chemvue na jeshi lake walienda kuvamia Nyamirembe mpambano ulikuwa makali mno.

Chemvue alipoteza askari hodari wa Baba takribani mia mbili Chemvue aliamuru kurudi nyuma ili wajipange upya Nyamirembe ilikuwa tayari imeisha kwa taarifa ya wapelelezi na ule msemo wa wahenga umetimia Uji ujauonja, tayari ushajua sukari yake” Chemvue aliamini atashinda vita kwa urahisi kumbe alisahau neno moja kuwaVita si sawa na kubwiya buyu.

Hii ilikuwa vita ya kwanza ya Chemvue kuiongoza na alipigwa kwelikweli alibaki analia kwa uchungu mkubwa kwani silka yake hapendi kushindwa kitu, alijiuliza mara kadhaa “kwanini nimeshindwa” pasipo kupata jibu alisahau kuwa” Chombo cha kuzama hakina usukani.

Mji wa Chimve ulikuwa kimya na hofu kubwa kwa kutoweka kwa watoto wa Chifu Gwindwa na Askari hodari wa vita wakitambulika k**a Jeshi la jenga.

Jeshi hili ni jeshi lenye kila kitu kuanzia uchawi na mbinu za kivita, Baba yake Chemvue alikuwa na hasira kwa kitendo cha watoto wake kutoroka na jeshi lake pia maisha ya wanae anajua yapo hatarini kwani anawajua wanae wanapenda mapigano hasa Chemvue.

USIKOSE TOLEO LINALOFUATA JUU YA MAISHA YA WATOTO WA CHIFU NA JESHI LA JENGA.

INAENDELEA...............

Address

Pembamoto
Dodoma
±255

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Simulizi za Mude posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Simulizi za Mude:

Share

Category