Hadithi Tamu

Hadithi Tamu Hadithi tamu ni tovuti maalumu kwa hadithi za Kiswahili na Kiingereza. Tembelea tovuti hii usome sto

James & Jennifer - Familia ya Siku TanoKupata mwendelezo wa hadithi hii/kitabu chote tafadhali wasiliana nami kwa WhatsA...
02/01/2019

James & Jennifer - Familia ya Siku Tano

Kupata mwendelezo wa hadithi hii/kitabu chote tafadhali wasiliana nami kwa WhatsApp 0764688786.

SURA YA KWANZA - JUMANNE.
Ilikuwa majira ya mchana jijini Dar es Salaam. Joto lilikuwa kali, kila anaetembea mkononi ameshika kitambaa akifuta jasho, au gazeti akijipepea. Gari dogo aina ya Toyota IST jeusi lilisimama, kisha mwanamume wa makamo alishuka pole pole. Mkononi alishika mkufu mdogo akiuchezea chezea. Macho yake yaliitazama shule ya msingi iliyo mbali kidogo.

Adam aliitazama saa yake ya mkononi, kisha akainua macho kuitazama shule. Alijifuta jasho kwa kiganja, kisha akarudi ndani ya gari. Hapana chezea joto la Dar, k**a una AC lazima uifuate. Akiwa ndani ya gari, Adam anainama, anatoa picha ndogo kwenye wallet yake na kuitazama. Picha hii ni ya mwanamke mrembo, aitwaye DIANA. Adam aliitazama picha kwa muda, akiwa na mawazo kichwani, huku anapitisha vidole vya mkono wa kulia taratibu akiipapasa.

Kisha alitoa picha nyingine ndogo. Hii ilikuwa ni ya watoto wawili mapacha wa kiume na k**e. Anaitazama kwa muda. Anazishika kila moja na mkono wake na kuzitazama kwa zamu k**a anazifananisha. Anatazama picha ya watoto na kuinua macho kutazama shule.

Adam anarudisha picha. Anatoa mkufu na kuutazama tena anainua macho kuitazama shule. Wanafunzi wanatawanyika kwa mbali.

Kundi kubwa la wanafunzi walikuwa wakikimbia kutoka upande wa shule, ilionekana ni muda wa kurudi nyumbani. Wanafunzi wawili wa k**e (JENNIFER) na kiume (JAMES) walikitembea kutokea shuleni.

Jenifer alitembea akicheza na kuruka ruka. Kisha, alikimbia mbele ya kaka yake. Anageuka kurudi kinyumenyume akicheza singeli. James aliishia kutingisha kichwa akicheka tu.

Adam anawasha gari na kuwafuata James na Jennifer polepole. Anawakuta mbali kidogo na shule. Anasimamisha gari pembeni yao. Jennifer na James wanasimama. Kioo cha gari kinashushwa na sura ya Adam inaonekana.

JENNIFER

Shikamoo we mbaba

ADAM

Marahaba, za shule?

JENNIFER

Nzu…….

James anamshika mkono Jennifer na kumvuta kuanza kuondoka. Adam anasogeza gari polepole na kusimama tena mbele yao.

ADAM

Hebu simameni, nyi ni James na Jennifer Mahinya?

JAMES

Ndio ni sisi, we nan na unataka nini?

ADAM

Mi ni afisa wa polisi,mama yenu ameniagiza. Ingieni niwapeleke alipo.

Adam anatoa pochi yake na kuifungua akiwaonyesha kitambulisho.

JAMES

Amekutuma mama?

ADAM

Ndio, amese…..

JAMES

Amesemaje? Kwani akutume wewe? mwenye yuko wa?

ADAM

Kuna ajali ndogo imetokea, mama yenu hajaumia ila amepumzishwa

Muhimbili.

JENNIFER

Anaendeleaje? imekuwaje?

ADAM

“Kuna moto ulitokea saloon kwake, hajaungua ila moshi ulimfanya azimie kwa muda, kaniomba niwapeleke Muhimbili.”

Jennifer anasogea karibu na gari. Anashika mlango wa gari kutaka kuingia. James anamshika mkono na kumvuta nyuma yake.

JAMES

Ngoja Jenny, k**a we polisi mbona hujavaa nguo za kipolisi?

ADAM

Kwenye kikosi chetu hatuvai sare, umeshawah kuskia askari kanzu?

JAMES

Ndio nawajua, mi sikuamini, nimeskia watu wanaiba watoto wanatengezea mafuta ya ndege.

Adam anatabasamu, kisha anacheka

ADAM

Hapana James, haiwezekani kutumia mwili wa mtu kutengeneza mafuta ya

ndege, mafuta ya ndege yapo ya aina tatu Jet A, Jet A 1 na Jet B,

yanatengenezwa kwa kuchanganywa, Hydrocarbons mbalimbali zenye

molecular weight tofauti tofauti, sawa eh?

JENNIFER

Unatumia maneno magumu magumu tusielewe enh? kwanza kwan we rubani?

ADAM

Si nimewaambia mi ni afisa wa polisi? mbona mnakuwa na maswali

mengi mengi? ingieni garini twende, au nikamwambie mmekataa?

JAMES

Hapana, tunataka uhakika kuwa kweli amekutuma, mpigie simu tuongeee nae.

ADAM

Unategemea saloon yake imeungua, ye…ametoka kazimia atakuwa amekumbuka

simu?….huh?

JAMES

Mhhhh sawa ila alituambia akimtuma mtu atamtajia jina maaalumu, we

kakwambia jina gani?

ADAM

Kasema nije kuwafata kunguru wake wa Zanzibar

JENNIFER

Hapo sawa, twende James kweli mama kamtuma.

Jennifer anafungua mlango wa nyuma na kuingia, James anafata polepole pole nyuma yake na kuingia. Adam anawasha gari na kuondoka taratibu. Gari inasimama nje ya duka kubwa la vyakula. Adam anageuka kuwatazama James na Jennifer waliokaa viti vya nyuma.

ADAM

Shukeni niwanunulie chochote cha kula, najua mtakuwa na njaa.

JENNIFER

Utamdai mama hela au huruma zako tu we mbaba? Mr…

Jennifer anainua mkono akimtazama Adamu na kupiga saluti anapozungumza.

JENNIFER (CONT’D)

Mr…Mr…Policeman

ADAM

ADAM, naitwa Mr ADAM MOSHA aya twendeni.

Wanashuka wote watatu na kuelekea kwenye mgahawa. Wanakaa na muhudumu anasogea.

ADAM

Tupe chipsi kuku kwa ajili ya Jennifer hapa na ubwabwa maini kwa ajili ya James.

JENNIFER

We mbaba mchawi nini, umejuaje hivo ndo vyakula tunavovipenda? James tumkimbie huyuuu, tumekutana na shetani.
Jennifer anasema akimtazama Adam na James kwa zamu. Kisha ananyanyua mikono na kutengeneza makucha kwa vidole vyake k**a paka akimtishia James anapotamka shetani. Adam anacheka kwa nguvu, anamtazama Jennifer kwa mapenzi makubwa.

ADAM

You are so funny Jennifer, umesahau mimi ni polisi? Tena polisi mpelelezi, tukiwa

chuoni tunafundishwa Psychology, jinsi ya kumsoma mtu bila hata

kumuuliza chochote, kwa mfano hapa nimekutazama machoni nimejua unapenda nini.

Jennifer anashika shavu lake na kufikiria kidogo, kisha anainua uso.

JENNIFER

Mhhh k**a kweli niambie, mi napenda rangi gan?

ADAM

Mhhh ngoja niwaze kidogo…. Okey umebeba beg la pink, niliona kalamu

yako ya pink pia ndani ya gari, ulipokuwa unaingia garini niliona

pia umevaa tight ya pink, naamini hata uniform mngekuwa mnaruhusiwa

ungevaa ya pink pia, so rangi uipendayo ni pink, uwongo uwongo?

JENNIFER

Duh we mkali unachungulia hadi watoto

Wote wanacheka, Adam anaonekana kuwa na furaha zaidi. Muhudumu anawaletea chakula.

MUHUDUMU

Samahani kaka, we hukuangiza chochote?

ADAM

Oh usijali, niletee Juice na Sambusa k**a mnazo

Muhudumu anaondoka, Jennifer anainua uma na kumuelekezea Adam.

JENNIFER

Usiwe unapenda kula sambusa we mbaba polisi umeskia eh?

ADAM

Kwanini mwanangu? mbona nzuri tu?

Jennifer anainua mkono na kuuweka k**a anataka kumnong’oneza Adam. Adam anasogeza kichwa.

JENNIFER

Ujue siku izi kuna mgao wa umeme kwa hiyo mashine za kusagia nyama hazifanyi kazi,

ADAM

Mh sijajua hilo linahusiana vipi na kusema nisile sambusa.

JENNIFER

Mapolisi wa siku izi bwana, wanataka kufundishwa kila kitu yan

Adam anacheka. Anatoa notebook na peni kwenye mfuko wa shati na kujifanya anaandika anachosema Jennifer.

ADAM

Ujue ukimdhalilisha polisi nina haki ya kukuk**ata? Lakini kwa kuwa

kweli sijui aya nakusikiliza mwalimu, nimeshakaa tayari na kuandika ufundishacho.

JENNIFER

Ni hivi, k**a mashine hazifanyi kazi manake wanashindwa kusaga

nyama kwa hiyo wanakodi watoto wawe wanatafuna nyama ila hawamezi

wanatemea kwenye beseni had zijae ndo wanaenda kutengenezea sambusa.

Adam anacheka sana, muhudumu aliekuwa kasimama nyuma ya Jennifer akimsikiliza anacheka pia. Jennifer anageuka anashtuka anapomwona na kuziba mdomo wake kwa mkono. Muhudumu anaweka Juice na sambusa za Adam mezani na kumpiga Jennifer na tissue papers alizokuwa nazo mkononi. Kisha anageuka na kuondoka.

Wanaendelea kula taratibu. Wanamaliza na kurudi garini. Wanaingia na safari inaanza tena.

ADAM

Okey, so watoto wazuri, mna mpango wa kuwa nani mkiwa wakumbwa? Jenny?

JENNIFER

Mh nina mpango wa kuwa Jenny mkubwa

ADAM

Hahahah aya umeshinda, una mpango wa kufanya kazi gani?

JENNIFER

Wakili

ADAM

Mwanasheria? kwanini?

JENNIFER

Ujue siku unapopata leseni ya uanasheria unapata na leseni ya

kudanganya.

Adam anacheka, anageuka nyuma na kurudisha macho barabarani.

ADAM

Mhhhh ila we unawezaje kujua wakili anadanganya?

JENNIFER

Mbona rahisi tu, ukitaka kujua wakili anadanganya angalia utaona

mawakili wenzake wanavutiwa na anachosema, au unamsikiza tu kwa

saabu vyote anavosema ni uongo tu

ADAM

Hahahahah haya Jenny! na James je? unataka kufanya nini ukubwani?

James anaonyesha kuboreka, anatazama nje na kuona mabango yanaonyesha wanaelekea Morogoro, anashtuka na kuangalia nyuma. Anainama mbele.

JAMES

We mbaba, hi sio njia ya Muhimbili, hii njia ya Kibaha, turudishe kwa

mama, unatupeleka wapi??

ADAM

Tunaelekea nyubani kwangu

JENNIFER & JAMES

Wapi????????

ADAM

Nyumbani kwangu

James na Jennifer wanatazamana. Kisha wanakumbatiana. Jennifer anaficha uso kifuani kwa kaka yake.

USIKU: SEBULENI KWA DIANA

Diana amekaa kwenye kochi. Anasimama na kuzunguka zunguka sebuleni. Anashika simu na kuiweka mezani tena. Anainua macho kutazama saa ya ukutani. Inaonesha ni saa mbili na nusu usiku. Simu ya mezani inaita. Anakimbia haraka na kuinyanyua

DIANA

Hallo!..hallo!…hallo!

Amesimama na simu ukutani hasikii chochote

DIANA

Hallo, we nan? k**a huna watu wa kuongea nao, piga simu redion

uongee na watangazaji, we mlinzi huna wa kuku kampani nini?

Diana anainua mkono mwingine usio na simu na kuikata. Kisha anarudisha mkono wa simu na kugeuka. Simu inaita tena. Anainyanyua kwa hasira.

Adam amekaa ndani ya gari ikiwa na mwanga mdogo. Ameshika simu kwa mkono wa kushoto ikiwa sikioni. Mkono wa kulia ameshika picha ya Diana akiitazama sana.

DIANA

We nani usie na kazi ya kufa…..

ADAM

Diana, mi ni Adam!

DIANA

Adam, Adam yup, yule alieshawishiwa na Eva au? unataka nini kwangu?

ADAM

Diana, ninao watoto!

DIANA

Whaaat? We unanjua unanskia?

ADAM

Diana, ninao watoto, ninao watoto wetu!

DIANA

Hiv we mzima kweli, una watoto na nan? Nataka wanangu kabla sijaita

polisi, we nan lakini?

ADAM

Mimi ni Adam, umenisahau? Lazima ulijua nitarudi.

DIANA

Nimesahau? Sijakusahau ila sikujui kabisa, and this is not funny, got it?

ADAM

Baba wa watoto, baba wa kweli wa Jenniffer na James. Diana anatoa macho, anapooza gafla anatereza ukutani pole pole na kukaa chini, simu akiwa kaishikilia begani.

ADAM

Diana, are you okay, nijibu please.

Diana analia taratibu, hajibu kitu mkono mwingine amejishika kichwani, machozi yanamdondoka

ADAM (CONT’D)

Diana, mbona hujibu? Kumbuka ninao watoto, naweza kuwafanya chochote

k**a tusipoelewana.

DIANA

Kwa nini lakin, kwa nini unanifanyia hivi? uliyoisha fanya hayatoshi?

ADAM

Nakupenda Diana, daima nimekupenda, nawapenda na wanetu pia,

nataka kuitunza familia yangu

DIANA

Jaman please, warudishe wanangu, nakuomba nipo chini ya miguu yako.

Adam ameshika simu, hajibu kitu, anaonyesha huzuni. Diana anasimama na kutembea tembea sebuleni. Anapaza sauti

DIANA

Nataka wanangu, unaskia we mbakaji, nataka wanangu nasema ntakufanyia

kitu mbaya wewe ohoooo.

ADAM

Diana! kunifokea hakusaidii, wapo salama nyumbani kwangu,

wapo nyumbani kwetu, kwako na kwangu.

DIANA

Unataka nin kwangu lakini?

ADAM

Nataka uje, uje tutengeneze familia pamoja, kumbuka ukitoa taarifa polisi au

kwa mtu mwingine yoyote, hutawaona watoto tena, nakupenda

sana Diana,

DIANA

Upo wap niwafate?

ADAM

Hapana! siwezi kukuambia kwa sasa.

DIANA

Adam, watoto wako wapi nataka kuongea nao, mpo wapi niwafate?

ADAM

Hapana haiwezekan! muda huu bado wamelala nyumbani.

DIANA

Umewaacha na nani, wako peke yao? Nataka kuona wanangu jamani!

ADAM

Haswaa utawaona usijali! na ndio sababu nimekupigia, kwanza hakuna

litakalo kuwa sawa bila uwepo wako.

DIANA

Itabidi nijue mpo wapi

ADAM

Ntajuaje k**a hutawaambia watu wengine? Au kuja na polisi kabisa?

DIANA

Adam, siwezi kufanya hivyo, k**a polisi ningeshatoa taarifa tayari! siwez kufanya hivyo, ntahatarisha, maisha ya wanangu, nipo tayari kwa lolote kupata wanangu.

Adam ameegemea gari. Anatembea taratibu na kurudi kuegemea gari. Mazingira na porini na kweusi sana. Hajibu kitu kwa muda.

DIANA

Jaman, please mbona hutaki kunielewa?

ADAM

Diana, nasikitika we ndo hutaki kunielewa, nataka uwe ni uamuzi wako

sio wangu. Sitajaribu kukulazimisha kuja, nipo tayari kukusubiri hata maika ishirini,

ila siku ukija inakuwa moja kwa moja. I want this to be right.

DIANA

Ila nataka kuja, nataka kuwa na wewe, nataka kuwa na familia yangu yote.

ADAM

Unamaanisha lakini Diana? huwa Sina masihara kwenye uwongo.

DIANA

Sijawah kuwa serious k**a leo maishani mwangu.

ADAM

Sawa k**a ni hivyo, sa ivi ulale kwa amani, watoto wapo salama, ntakupigia simu

sa moja asubuhi kukuelekeza, kumbuka, No police and everything will be okay, I love you

DIANA

Nataka kuongea nao….. hallo! ngoja usikate si… hallo! hallo!

Kupata mwendelezo wa hadithi hii/kitabu chote tafadhali wasiliana nami kwa WhatsApp 0764688786.

01/11/2018

Ushosti Lawama - Hadithi Fupi (fiction)

Mama Haika alikua akitembea haraka, akihangaika kuokota khanga yake inayokaribia kuanguka japo ana mwili mkubwa, na chura mmoja matata sana. Naposema chura sio hawa wa vidimbwini mvua zikinyesha. Chura chura haswaa, kitu Goliath Frog (najua hujui, fanya kuGoogle uongeze maarifa).

Mama Haika aliendelea kutembea haraka, huku akihema k**a anakaribia kupiga cha pili, maana cha kwanza kile huwa na kiherehere k**a konda kuruka kwenye gari kabla haijasimama. Alipiga kona ya kwanza, ya pili, kisha ya tatu…akaibukia kwa mama Almasi. K**a bahati nzuri au mbaya, Mama Almasi nae alikua nje ya nyumba yake. Kainama anafagia.

Huyu alikua wa tofauti kidogo, alikua na kamwili kembambaa wenyewe mwaita vimodo sijui, wengine mara Size Zero. Naposema mdogo namaanisha hana nyama, hakuna pa kushika. Akivaa dera anakua k**a kichuguu.
‘We kimbaumbau k**a mdoli wa boutique wa kuniibia bwanangu wewe’

Alifoka Mama Haika toka umbali wa mita k**a kumi hivi.
‘Weee koma, ishia huko huko na huo mdomo…ntakubamiza nikamue mafuta hayo nipikie vitumbua’
Alijibu mama Almasi.

Hakujaliwa uzuri, wala shepu, wala urefu, wala mwili. Ila mdomo sasa, ni k**a Mungu alimnyima vyote akavichanganya mdomoni, mwanamke alikua anajua kuongea. Mtaa mzima hakuna.

‘Weee, uanzie wapi, kwa mwili gani. Hebu mwone, ndio maana mfupi hadi ukipiga Selfie unatoka mwili mzima’

Alijibu kwa jazba mama Haika. Alikua keshafika uwanjani kwa Mama Almasi.

‘Halululuuuu, Mi siongei mwenyewe barabarani...labda nikiwa kwenye kioo..najitamani’ Mama Almasi alijigamba, ukimwona mtu mwenyewe sasa.

Mama Haika: Unajipost au unaLIKE....kwa bundle gani??
Mama Almasi: Hiki hiki kifurushi cha chuo kimemtoa bwanako huko…kaja kukifata college, na gari alipak hapo uliposimama.

Mama Haika: Weee hebu nyamaza, na kamwili hako utakua umemroga tu.

Mama Almasi: We k**a bulldozer tu, kugeuka nyuma tu mwaka….Ukigeuzwa kitandani na godoro linageuka
Mama Haika: Hivi we unajivunia nini, kwanza ujue aliegundua dera aliona mbali, watu wenye miguu k**a nyie mngetembeaje barabarani?

Mama Almasi: Hahahha haluluuuuu! kukaa karibu na godown sio kupat kazi shoga, uwe na tako k**a boneti la lori mumeo tunamuiba tu!

Mama Haika: Mwanamke una roho mbaya hadi shetani anakuomba ushauri…kweli shoga umenizunguka.
Mama Almasi: khaa shoga umekuja moto, we nan kakupa huo ubuyu…bwanako mwenyewe kimbaumbau mwenzangu yule Tukikumbatiana tunakua ka tambi za Santa Maria?
Mama Haika: (Akicheka) hata mi nilitaka kushangaa, si Swaumu ndio kaja kanambia na maziwa yake juu juu k**a k**a anaweka luku mita ipo juuu
Wanacheka na kugona mikono.
Mama Almasi: Huyu Swaumu kila siku nakuja kudowea chai hapa ndio anataka kutochonganisha?
Mama Haika: Heee, ndio. Mi nikajua huwa anakuja kwangu tu.
Mama Almasi: Katoka hapa sio muda, nimempa chai na mihogo hata bakuli hiyo hajaisogea

Wanacheka tena kwa nguvu
Mama Almasi: Nimempa chai moto muhogo moto na pilipili k**a nna shamba hivi
Mama Haika: Shoga angu we mtata ujue!
Mama Almasi: na kwambia yuko enh enh enh anahemea mdomo tu… kaungua ulimi..namwambia basi tema k**a unaungua…eti ohoooo tema niteme utamu, namwambia basi meza basi muhogo ...huyooo anajibu wa moto ntaungua utumbo……nampa maji anyweny……ah ntaharibu ladhaaaaa
Wacheka na kugona mikono. Mama Haika anakaa kwenye mkeka. Mama Almasi akihangaika na dera lake k**a mfuko wa mashine ya kusaga.

Kupata story nyingine fupi fupi k**a hizi, LIKE page yetu.

ChatmateSehemu ya Pili‘Khaaa… nitumie nauli nije kumchamba, tuma nauli nije kulianzisha sasa hivi’‘Hapana mama….we acha ...
30/10/2018

Chatmate
Sehemu ya Pili

‘Khaaa… nitumie nauli nije kumchamba, tuma nauli nije kulianzisha sasa hivi’
‘Hapana mama….we acha tu!’
‘Ndio tatizo lako hilo mwanangu… upole upoleee ndio maana wanakupanda kichwan, wanaume sio watu mama…ukileta ulegevu utaonewa hatari…kwanza sio lazima kuolewa’
‘ila mbona we umeolewa miaka ishirini na tano sasa!’
‘mh hilo nalo neno! Mwanangu pole…utapata tu mwingine wa kukupenda kweli! Achana nae kwanza alikuwa na meno mabayaaaa’
‘mama we unamjua?’
‘Ah nimehisi tu, wanaume wenye meno mabaya huwa na kisirani k**a nini’
‘Ila kwanini mim tu mama…nakaribia miaka thelathin, kila mwanaume anakuja akipata anachotaka…huyoooo anakimbia…mi ntakaa hivi mpaka lini?’
‘Pole vumilia tu mwanangu! Mungu yupo!’
Kimya kwa muda!
‘hivi we umeachika kweli, au ndio maneno yako nisipate luku mie’
Sarah anacheka kwa muda! Kisha;
‘Haya mama ngoja niende kwa wakala…nitumie mita namba basi’
‘Heee! Yan umetuchoka hadi umefuta, na sie tumezidi’
‘hapana mama, ile simu si alinunulia Oscar! Aliponiacha…alinyang’anya akampa huyo mwanamke wake mpya!’
‘Tobaaaaa! Hadi simu…mwanangu omba ruhusu uje twende kwa yule mzee tukamtengeneze! Hawezi kukufanyia hivi!
‘Mama si umetoka kusema nivumilie mungu yupo?’
‘Mmmmmh we nawe kujifanya binti mlokole, haya kata nikutumie hiyo namba…nisije sema mengine bure! Na joto hili tutaota fangasi kwenye naniii…maana!
‘mama?’
‘Pole mwanangu…unitumie mwingi mwingi nisisumbue tene eeeng’
‘Si ulisema wa elfu mbili wewe!’
‘Ndio maana unaachika, unashindwa kusoma alama za nyakati’?
‘Mama!’
‘Hutaniwi? Kwa heri?

Kupata mwendelezo wa hadithi hii tafadhali LIKE Page yetu.

Hussein Tuwa ni mwandishi mashuhuri kutoka Tanzania. Ameandika vitabu mbalimbali k**a vile Mkimbizi, Mtuhumiwa, Mfadhili, Mtafiti, Bondia na Utata wa 9/12. Hussein anajulikana zaidi k**a bingwa wa Taharuki.

30/10/2018

Chatmate
Sehemu ya Kwanza

Griiii griiii griiiiii
Griiii griiiiii griiiii
Smartphone kali iliendelea kulia
‘Oyaaaa, fanya kupokea au iweke silent, inatuharibia concentration’ ilisikika sauti toka nyuma ya computer nyingi zilizoko hapo ofisini.
Sarah, akashtushwa kwenye mawazo yake…kuangalia simu. . Kwenye kiooo, kuna picha ya mama mtu mzima amejitanda khanga, jina lilionekana Dear Mommy.
‘Hallo, mama!’’
Alipokea Sarah, huku akifuta futa k**asi na machozi kwa mbaaali yaliyokuwa yakimtiririka, bila kujua. ‘Mwanangu, kwema…mbona sauti kavu k**a yule mbunge Halima sijuiii…kulikoni?
‘Ah mama acha tu, vipi wazima huko?’
‘Ah sie tuna shida zetu, ila nambie kunani?’
Sarah alikaa kimya kidogo, akivuta vuta mafua. Kisha;
‘Hamna mama, basi tu mambo ya kazi, niambie kipenzi….kunani huko, maana si kawaida yako kupiga simu saa kazi, kwema?’
‘Ah huku wazima, sema wenzio umeme umekata luku! Tutumie hata wa elfu mbili tu tuwashe feni, maana si kwa joto hili’
‘Hee poleni, sasa kwenye simu sina hata mia…SIMBanking nayo imekauka k**a kwapa ya mzee, si unajua tarehe hizi….vumilieni kidogo basi, nikitoka kazini ntawatumia’
‘Haya’ mama alijibu kionyonge.
‘Bibi weeee mbona unajibu k**a nyau kamwagiwa maji’
‘Ah hamna, maana pana wageni hapa jasho linawavuja hatari….wapo chapachapa k**a ku** ya mwanamke wenye ukame wa mwaka’
‘Haaaa mama ushaanza hivo na maneno yako, hivi mi binti yako ujue’
‘Kwani uongo? We huwa inakuaje ukishaona ile naniluu ya mkamwana usiyetaka kumleta’
Sarah alikaa kimya kwa muda…kisha;
Akilia ‘mama Oscar kaniacha, ana mwanamke mwingine!
‘Heee ndio kisa cha kuwa mnyonge hivo, mwanangu mi nilishakwambia wanaume wote baba yao mmoja, muweke moyoni nusu usiingie kichwa kichwa….haya ilikuaje?’
‘Jana siku nzima hajanitafuta, napiga simu hapokei…kwenda kwake nakuta yuko kifuani kwa mwanamke mwingineee…’

Inaendelea Post inayofuata. Tafadhali share na wengine waione.

Kisura wa InstaSehemu ya TatuNikazama DM..’Good evening, I am writing on behalf of Aphrodite Modeling Agency, we will be...
30/10/2018

Kisura wa Insta
Sehemu ya Tatu

Nikazama DM..’Good evening, I am writing on behalf of Aphrodite Modeling Agency, we will be interested in interviewing you later this week for Television Advert to one of the reputable telecom company. If you are interested, please let us know’

Hapo hachomoki, kwa deal hiyo hata iweje…anaanzaje sasa kuchomoka? Account niliyokuwa natumia ni mahsusi for that, imetengenezwa k**a Agency, kila siku ni kujaza mipicha ya behind the scene ya uongo na kweli…naenda Ghana huko nachukua mipicha ya fasheni naijaza, ukiona akaunti unaona ah kesho tu unatokelezea kwenye Vogue magazine, kumbe hamna kitu.

New sms…hawachelewagi hawa! ‘Hi thenk tyu ver much for the opportunity. Hiya is my numbe +2557186****6.
Lahaula, hahahhaa hata sijatumia nguvu nyingi…Magu mbaya, watoto wana njaa vepe!. Sasa huyu lazima aliwe le oleo. Baada ya kuwa na namba, sio ishu. Nikazama kwenye simu, nikamtumia misimbazi kadhaa. Kisha nikachill kwa muda.

Baada ya dakika kadhaa nikamwendea hewani, “Hello mambo’’
Hallo? Za kwako
“Poa, sorry nilikua namtumia mtu hela bahati mbaya ikaja kwako” “ah enh nilikua na shida nimeshatoa, nita…nita…’
‘Oh hakuna shida usijali’
‘Ah sasa’
‘Usijali, ni makossa yangu mwenyewe! By the way una sauti nzuri sana… we ni mtangazaji wa redio?”
‘Oh hapana, ndio kwanza mwanafunzi’
‘Okay, nimefurahi kuzungumza na wewe! Upo wapi kwani?’
‘Tabata’
‘Oh mi niko Sinza, k**a hutajali…may be tunaweza kuonana nikakuongezea nyingine kidogo’
Kimya! ‘Hallo, upo?’
‘Yeah, ila saivi…’
‘Sio lazima saivi…nicheki jioni basi’
‘Sawa I will’
Nikakata simu tabasamu usoni. Ukiona manyoyaaaaa?

Mwisho. Tembelea www.hadithi.co.tz/index kusoma hadithi zaidi.

Hussein Tuwa ni mwandishi mashuhuri kutoka Tanzania. Ameandika vitabu mbalimbali k**a vile Mkimbizi, Mtuhumiwa, Mfadhili, Mtafiti, Bondia na Utata wa 9/12. Hussein anajulikana zaidi k**a bingwa wa Taharuki.

30/10/2018

Kisura wa Insta
Sehemu ya Pili

Oh My GOD.

Nilijikuta nikiropoka kwa sauti…watu wawili watatu waliokuwa meza ya jirani waligeuka na kunitazama. Macho kwenye simu, sikuamini kile nilichokiona, kwanza nikafikicha macho, kisha nikajiweka vizuri kwenye kiti, nikishusha sehemu ya mbele ya suruali kumweka Jongoo vizuri, maana alishaanza usumbufu. Macho kwenye simu, Ilibidi niZoom in kiasi kuona vizuri…kimya! Nikajaribu tena! Hakuna kinachotokea, gafla nikakumbuka…hakuna zoom in kwenye video. Nikajikuta nikipiga meza kwa nguvu, kwa hasira iliyochanganyika na mshangao.

Mtoto alikua akicheza wimbo wa Salome wa Diamond Platnumz. Hakuwa amesimama, anacheza kajilaza kitandani. Lakini huo ulaini wa kiuno hatari, kwa mbali cheni ya gold iliyofubaa ilikuwa inan’gaaa…ah mama weee, ugonjwa wangu huu mwenzenu…raha ya kiuno shanga.

Niliendelea kumtazama mtoto yule akinyonga taratibu, nikajikuta huyo kwenye profile. Mama MIA! Kulikuwa na video nyingi za aina hiyo, na picha nyingi alizopiga.

Zote zilifanana kitu kimoja, sehemu kubwa ya mwili wake mchanga…laini wenye kutia hamasa zilikuwa zinaonekana. Kwa kumtazama, si mtu mwenye pesa…nguo zake za bei rahisi, hata ukitazama hicho kitanda na mashuka ni yaleee ya bei zetu..but who cares? Kwanza kwa uno lile una muda hata wa kuangalia kitanda wakati utamu wote huu hapa?

Inaendelea Post inayofuata.
Tafadhali, tupe maoni yako kwenye comments

30/10/2018

Kisura wa Insta
Sehemu ya Kwanza.

Ilikua ni siku ya jumamosi, siku nzuri ya kuzurura bila kwenda kazini. Jana yake nililewa kiasi, nikaona isiwe ishu ngoja niende baa ya jirani na home nikapate walau supu. Mwanaume misosi vinginevyo game za kibabe za chumbani zitakushinda, utajikuta unahema ulimi nje k**a umelamba mchanga.

Basi ile kuingia kwenye gari, nikashtukia kuwa ni chafu balaa, vumbi k**a kwa fundi seremala. Sio ishu, ntaiosha pale pale. Moja mbili moja nikajikuta nipo Sinza. Nakunywa supu, huku jirani wanasafisha gari. Baada ya kumaliza paja langu la kuku na ndizi, kitumbo ndii k**a mimba changa, nikajikuta sina cha kufanya. Nikaona isiwe ishu, acha niingie mitandaoni nikashangae shangae.

Nikaanzia Twitter, timeline imepoa hakuna shida. Nikaingia Jamii Forums, dah wamejaa wanasiasa tu wanabishana mara hiki mara kile. Get a life! Kisha nik**alizia zangu Insta, kijiwe cha watoto wakali. Nikaanza na vijivideo vya moments, watu wakonyesha walichofanya jana…mara maMoet mara Manini sijui, show off tu hawana lolote, wamejichokea tu. Kisha nikaenda sehemu niipendayo kuliko zote.

Search!
Hapa ndio huwa naona watoto wapya, maana Insta wanakupa suggestions, utaona mapaja hapo ya kila size. Nikajiweka vizuri kwenye kiti, huyo nikaanza kuperuzi, sura ipo makini k**a jaji anasoma hukumu, kumbe naangalia vichucho tu vya watu, simu zina mengi hizi hatari. Nikaendelea hivyo kwa muda, kisha! Lahaula, there she was, the one and only….jina refu k**a mabasi ya mwendokasi… ila chombo moja mamata sana.

Itaendelea, nipe maoni yako kwenye comments.

Address

8854, Mbezi Beach
Dar Es Salaam
25500

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Hadithi Tamu posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share