06/06/2026
Kwenye kitabu cha Alchemist wakati Paulo Coelho anatupeleka kwenye safari ya kijana Santiago, kuna somo moja kuhusu kitu kinaitwa “Biginner’s Luck”. Bahati ya mwanzo wakati unaanza. Ukiwa unaanza mambo huonekana marahisi, lakini baada ya muda hali hubadilika. Niweke nukuu moja kabla ya kuendelea;
“Every search begins with beginner’s luck. And every search ends with the victor’s being severely tested” Alchemist, by Paulo Coelho
Sasa turudi kwenye somo👇🏾
“Most people don’t fail because the dream is impossible. They fail because they quit when they finally discover how difficult it is.”
Kwenye mahojiano, Aliko Dangote wakati anazungumzia kiwanda chake cha kusafisha mafuta amesema kitu ambacho kila mjasiriamali na mfanyabiashara anatakiwa kukisikia.
Anasema kwa utani kidogo:
“Luckily for us, we didn’t know what we were building.”
Halafu akaongeza kwamba k**a angeonyeshwa ukubwa wote wa mradi wa refinery, drawings zake, complexity yake na changamoto zake zote siku ya kwanza, huenda asingethubutu kuanza kabisa.
Hapa unajifunza nini?
Watu wengi wanapenda matokeo makubwa, lakini hawajui ukubwa wa matatizo yaliyokuwa nyuma ya matokeo hayo.
Dangote anaendelea kutoa mfano mzuri sana:
“It’s like you’ve started swimming across the ocean.”
Yaani umeanza safari. Ukifika katikati ya bahari ndipo unagundua mawimbi ni makubwa kuliko ulivyodhani.
Ukigeuka kurudi nyuma ni mbali.
Ukiangalia mbele nako ni mbali.
Hapo huna option nyingine isipokuwa kuendelea kuogelea.
Kuna soma hapa kweli?
1. “Maono makubwa hujifungua taratibu.”
Wakati mwingine Mungu au maisha hayaonyeshi ugumu wote wa safari mapema. Yangeonyesha, watu wengi wasingeanza kabisa.
2. “Commitment huanza pale excitement inapoisha.”
Siku za mwanzo kila biashara huwa na excitement.
Lakini waliofanikiwa ni wale walioendelea hata baada ya ugumu kuanza kuonekana.
3. “Kuna point ya kutorudi nyuma.”
Ukifika level fulani kwenye biashara, uwekezaji au ndoto yako, gharama ya kuacha inakuwa kubwa kuliko gharama ya kuendelea.
4. “Persistence ni competitive advantage.”
Watu wengi wana akili.
Wengi wana mtaji.
Wengi wana opportunities.
�