27/04/2025
allahummaghfirlaha warhamha wa sakkinhu fil jannah
Nimeondokewa na Mteja wangu wa nguvu, kipenzi changu, pepo yangu, Mama yangu Alhamdulillah. Muda mwingine mlikuwa mnaona napost abaya ndani ta dakika 5 sold out ni yeye alikuwa anaziwahi, wakati mwingine nilikuwa mpaka namficha asione mzigo mpya😃lakini alikuwa ananiwahi nikipost tu yumoo. Kwakweli alikuwa Bestfriend wangu mnoo. Kipindi nimeanza hii biashara nilitamani nipate jina la biashara hii, wengine husema Brand. Katika kutafuta nikaona niite majina ya mama yangu kipenzi na ndipo nilipata . MS ni herufi za mwanzo za majina yake la kwanza na la pili. alifurahi sana alivyojua maana ya MSabayastore. Nilikuwa namuomba Allah kilasiku ampe maisha marefu kumbe hakuwa na maisha marefu yale niliyokuwa nikiyataka mimi. kuna muda naona k**a ni ndoto nabaki kumshukuru Allah ni njia yetu sote. Sisi ni waja wake na kwake ndio marejeo yetu. Alhamdulillah.