02/03/2021
MAMA USINIFUNDISHE UCHAWI
SEHEMU YA TANO
Walipomaliza kula Sharifu akatoa vyombo akaenda chumbani na kumwacha mama yake kwenye mkeka pale ukumbini akishona khanga. Safari hii Sharifu hakutaka kusikiliza redio, alipofika kitandani akajitupa chali na kujibembeleza kwa kujitingisha miguu punde tu akapitiwa na usingizi.
Alikuja kushtuka mishale mingine kuchungulia dirishani akaona giza limetanda pande zote kuashilia usiku umeingia huku likisindikizwa na wingu zito la mvua na mweku mweku zikimurika na kuzima kuwa giza. Hali ile kwa mtu muoga asingethubutu kunyanyua miguu yake na kutoka nje.
“Giza hili, naona linaniruhusu kwenda kilingeni ngoja nikamwamshe mama,” Sharifu alijisemea nafsini kisha akajibadilisha muonekano akayayuka chumbani kwake na kutoka nje kuelekea kwenye mlango wa chumbani wa mama yake na hatimaye kuongea kwa hisia na mama yake.
“Amka mama.”
“Naona leo umewahi sio kawaida yako, ama kweli umepania,” Binti Mngane aliongea naye huku akijibadilisha muonekano mara baada ya kuamka.
“Ninashauku sana na wamama wale, si wanajifanya wanajua sasa leo watakiona cha mtema makuni,” Sharifu alizungumza huku akizungusha macho yake kimiujiza.
“Kweli dhahiri, umewapania.”
“Wewe, acha tu mama,” Sharifu alimsubiri kwa muda mama yake, ghafla akamuona mama yake ametokea kimiujiza alipo yeye. Akiwa tayari kashajiandaa wakayayuka pamoja tayari kuanza safari na kabla ya kufika kwenye tukio wakashauriana.
“Unavyoona wewe, tuanze wapi?,” Binti Mngane akauliza.
“Naona k**a vile kwa Mama Abuu ni karibu tuanze kwake, baadae tukishatoka kwa Mama Abuu ndiyo twende kwa Mama Stumai,” Sharifu alimjibu mama yake huku akitupa usinga huku na kule kwaajili ya kusafisha njia.
Waliposhauriana na mama yake wakaelekea moja kwa moja kutua kwenye uwanja wa nyumbani wa Mama Abuu. Walipotua wakashangazwa sana na hali waliokumbana nayo, wakakuta zizizi kumetulia huku kukichochewa na giza. Hali ile tulivu ikawafurahisha sana.
“Inaonekana Mama Abuu yupo kwenye usingizi mzito, lengo letu tulifanye haraka tuondoke,” Binti Mngane alimweleza mwanae huku akiusogelea mlango wa kuingilia ndani.
“Basi niache niingie ndani, kinachojiri nitakujuza,” Sharifu alimwambia mama yake huku akiegemea mlango wa Mama Abuu na kuyayuka kutokea chumbani.
Sharifu akamkuta Mama Abuu yupo kitandani amelala na mumewe usingizi wa pono. Akamchukua kimazingara mtuhumiwa wake na kutoka naye nje. Binti Mngane alipomuona mwanae amerudi na Mama Abuu kwa kumkokota k**a mkokoteni akafurahi sana.
“Naam!!!, huo ndiyo uwanaume,” Binti Mngane alimsifia mwanae mara baada ya Sharifu kufika alipo.
“Mtu wetu, huyu hapa,” Sharifu aliongea huku akimkabidhi Mama Abuu kwa Pilato.
Alipokabidhiwa kwa Binti Mngane akamwagiwa unga mweupe wa chengachenga unaofanana na mchanga unaosaidia mtu asiweze kuamka mapema. Akiwa hajitambui wala kuonyesha dalili ya kufumbua macho akawapa moyo na kuwafurahisha Binti Mngane pamoja na mwanae.
“Huyu mtu inaonyesha dawa tuliyompatia, itatufanya tufanye kazi yetu bila kipingamizi,” Binti Mngane alimwambia mwanae huku akipanda tumboni mwa Mama Abuu aliye na ujauzito wa miezi nane.
“Umejuaje?,” Sharifu aliuliza huku akimkodolea macho mama yake.
“Nimeona kuwa Mama Abuu, hana kinga.”
“Kwa hiyo tutafanikiwa, kufanya kazi yetu kwa uzuri,” Sharifu aliongea kisha kwa pamoja wakafurahi na mama yake huku wakicheza kwa kukata viuno kwa maringo.
Baada ya muda kadhaa Binti Mngane akafungua kitambaa cheusi kisha akatoa kimzizi chenye miiba mikali. Akakitemea mate kimzizi kile hatimaye akamlisha kinywani Mama Abuu. Walipohakikisha wamemaliza kumlisha kimzizi wakamrudisha Mama Abuu chumbani aendelee na usingizi.
“Mama Abuu dawa yake ipo jikoni inachemka, baada ya muda mfupi atainywa,” Binti Mngane alimweleza mwanae mara baada ya kumrudisha Mama Abuu.
“Nikiwa nawe nafarijika na kujifunza, mambo mengi sana mama yangu.”
“Yakupasa ujifunze mengi tunayofanya, ili baadae uweze kuwa mwanachama madhubuti,” Binti Mngane alimweleza mwanae huku akinusisha pua kila upande ajue k**a kupo shwari.
“Nitajifunza kila kitu kutoka kwako...lakini mama muda ushakwenda twende kwa Mama Stumai sasa tuk**alize kazi yetu,” Sharifu alimwambia mama yake mara baada ya kuona wanachelewa kwenda kwa Mama Stumai.
“Kweli tuondoke, tusije kuchelewa tukaumbuka kukipambazuka,” Binti Mngane safari hii alinusa juu ya anga kisha akamshika mikono mwanae na kuyayuka eneo lile.
Binti Mngane na mwanae wakaelekea nyumbani kwa Mama Stumai. Hali ya hewa kwa wakati ule ilionyesha anga ikiwa na mwanga hafifu huku nyota zikiendelea kumelemeta kwa mbali ikiashilia kuwa kunakaribia kupambazuka.
“Tushafika sehemu husika, nisubiri nje safari hii mimi niende nik**alize mchezo,” Binti Mngane alinong'ona mara baada ya kutua kwenye uwanja wa Mama Stumai.
“Ila kuwa makini, si unajua madhara ya hii nyumba?,” Sharifu aliuliza kwa kumhabarisha mama yake.
“Madhara gani tena? mbona unanitisha,” Binti Mngane aliuliza kwa kutaka kujua madhara ya nyumba ile.
“Wewe ushasahau, k**a Mama Stumai ni mrokole?.”
“Mmh!!! nilikuwa nimeshasahau, nitakuwa mwangalifu usijali kuhusu hilo mwanangu,” Binti Mngane alisema huku akienda ndani kinyume nyume mara baada ya kufungua mlango.
“Sawa, nitakusubiri,” Sharifu aliongea huku akizunguka nyumba ya Mama Stumai kwa kusota makalio kuhakikisha usalama.
Binti Mngane alipokaribia mlango wa kuingia chumbani mwa Mama Stumai akasotea mlango kwa makalio hatimaye mlango ukafunguka kisha akaingia chumbani. Alipofika chumbani akamkuta Mama Stumai akiwa amelala nafasi ile Binti Mngane hakutaka kuichezea.
“Wewe si mjanja!. Sasa leo nakuonyesha k**a kuna wajanja zaidi yako,” Binti Mngane alijisemea moyoni kwa kumtupia vijembe mzazi mwenzake.
Baada ya kutupa vijembe hakuchelewesha akanyoosha mkono wa kushoto mbele kisha likatokea pembe la ng'ombe.
Akampiga Mama Stumai miguuni na lile pembe, alipoona k**aliza mchezo bila kipingamizi chochote akajipongeza kwa kicheko hatimaye akayayuka pale chumbani na kutokea nje alipomwacha mwanae.
“Sasa kazi imekwenda vizuri bila kuchelewa tutoweke eneo hili kabla akujapambazuka,” Binti Mngane alimwambia mwanae kisha wakaondoka na kuja kutua kwenye uwanja wao wa nyumbani na kila mmoja akaingia chumbani kwake kujipumzisha kwaajili ya kuondoa uchovu.
**********
Asubuhi ya alfajiri mume wa Mama Abuu akawahi kuamka kwaajili ya kuwahi shamba k**a desturi yake ya siku zote, lakini alivyoamka akashangazwa na jambo aliloliona kwa mkewe.
“Wewe Siawezi,” Baba Abuu alimwamsha mkewe kwa kumpiga vibao.
“Kuna nini, Chang'ari?,” Mama Abuu aliuliza akiwa bado usingizini.
“Tumbo umelifanyaje?,” Baba Abuu alifoka na uso kaukunja k**a Nyati.
“Kwani lina nini?,” Mama Abuu aliuliza na hakuelewa mumewe ana maanisha nini kutokana kuwa alikuwa bado anaendekeza usingizi.
“Mtoto wangu wa tumboni umempeleka wapi?..ushaenda kumtoa kafara nini?,” Baba Abuu aliuliza kwa sauti ya juu huku akionyesha kuwa na hasira.
“Mungu, wangu!!!,” Mama Abuu alishtuka toka usingizini mara baada ya kuona ujauzito wake kupotea. Kisha akameza mate kwa muda na kumtazama mumewe aliyefura k**a mzoga wa Bata na kulijibu swali aliloulizwa.
“Mimi sielewi kitu,” Mama Abuu alijibu huku akijiangalia tumbo lake mara mbili mbili asiweze kuamini kilichotokea.
“Wewe mwanamke usinifanye sina akili, nina akili zangu timamu niambie mtoto yupo wapi?.”
“Sijui Chang'ari.”
“Nakuambia hivi kuanzia sasa sihitaji kukuona katika nyumba yangu mpaka pale utakapomrejesha mtoto wangu. Mwanamke gani unaendekeza ushirikina,” Baba Abuu alimfukuza mkewe kwa kumvuta atoke nje huku akimpiga ngumi za tumboni mara baada ya kuona mkewe mbishi kutoka ndani. Hakumsikiliza kabisa mkewe, akamfukuza mkewe k**a Mbwa aliyemlia mboga ya ngama.
**********
Mama Stumai akaamka asubuhi akiwa na furaha tele, lakini furaha yake ikaja kuzizima bila kutarajia mara baada tu ya kunyanyua mguu wake wa kuume na kuona umepooza.
“Looh!!!, nini tena hiki?,” Mama Stumai akajiuliza.
“Siamini, mbona haya maajabu nilale mzima niamke nimepooza,” Mama Stumai alijisemea huku akijikokota kushuka kitandani na kukaa sakafuni kwaajili ya kujinyoosha miguu athibitishe.
“Nimeamini uchawi upo japo sikuamini mwanzoni, kweli usilolijua ni k**a usiku wa giza,” Mama Stumai alizidi kusema na kujuta pale sakafuni. Furaha yake yote ikapotea kwa siku ile na punde tu akajikuta mwenye msongo wa mawazo. Akashindwa hata kujizuia kutoa chozi na asimuone wa kumfariji kwa nyakati ile ya matatizo kwake.
**********
Binti Mngane asubuhi na mapema akawahi kuamka na kuzifanya shughuli zake za nyumbani. Muda ulikwenda sana akaona mwanae hana hata dalili ya kuamka ndipo ikamlazimu aende kumwamsha.
“Sharifu, Sharifuu” aliita Binti Mngane kwa kupaza sauti.
“Naam!!!,” Sharifu aliitika kwa kukurupuka toka usingizini mara baada ya kuamka na kufikicha macho.
“Kulala gani hadi saa hizi?.”
“Nimechoka mama, niache nipumzike,” Sharifu alijibu kiuchovu kisha akajilaza tena kitandani.
“Mwenye usingizi peke yako, mbona nami nina usingizi ila nimeamka kufanya kazi...ebu nawe amka,” Binti Mngane alimwambia mwanae kwa kumlazimisha aamke.
“Naomba mama niache nilale kidogo. Nikiamka nitafanya hizo kazi,” Sharifu aliomba mama yake amwache alale kisha akavuta shuka akaendelea kulala.
“Lala ila jua, ukiamka kuna kazi zinakusubiri,” Binti Mngane alimuhabarisha mwanae kisha akaenda jikoni kupika. Baada ya masaa kupita Binti Mngane akawa kashaivisha uji na viazi vitamu. Akatenga chakula ukumbini kisha akaenda kumwamsha tena mwanae.
“Wewe, mtoto.”
“Naam.”
“Uji! tayari.”
“Nakuja.”
“Fanya haraka.”
Sharifu akatoka chumbani kwake mara baada ya kuitwa na mama yake huku akipepesuka k**a mlevi wa gongo kutokana na usingizi. Akajifikicha macho ili aweze kuona mbele vizuri. Akajikongoja taratibu hadi ulipo mswaki kisha akauchukua na kuelekea uwani ili kusafisha meno na uso nyuma akimwacha mama yake akimngoja ukumbini.
“Sharifu,” Binti Mngane alimuita mwanae mara baada ya kuona anachelewa kurudi.
“Na naam,” Sharifu aliitika kwa shida kutokana na mswaki kuwa kinywani.
“Huko kunawa, mwaka!.”
“Nakuja, ndiyo nafunga mlango wa uwani.”
“Harakisha bwana, tuje tule,” Sharifu punde tu alirudi ndani na kuketi kwenye mkeka ukumbini mara baada ya kuchomeka mswaki ukutani.
Walipomaliza kunywa uji Binti Mngane akatoa vyombo nje avioshe.
Sharifu akapumzika kidogo kisha akanyanyuka kwenye mkeka na kwenda kufagia banda la kuku. Akafagia huku akijiburudisha wimbo ambao aliwahi kufundishwa na baba yake kipindi cha nyuma kabla ya uhai wake.
“Mdooogo mwanangu mdogo...aowa owa,
Jisomeee mwanangu jisomee...aowa owa,
Uniokoooe mwanangu uniokoe...aowa owa,
Nakuombeeea baba yako nakuombea...aowa owa,
Kwa mwenyeeezi nakuombea kwa mwenyezi...aowa owa,” Sharifu aliimba nyimbo hiyo k**a mara mbili na kucheza kwa kutingisha kichwa na kunyanyua miguu.
Binti Mngane alipomaliza kuosha vyombo akaenda kwenye banda la kuku kumwangalia mwanae k**a anafagia au lah. Kufika akashangaa kuona mwanae akiimba nyimbo aliyoipenda kuiimba mumewe kipindi cha nyuma.
“Leo unafuraha, eenh?,” Binti Mngane aliuliza mara baada ya kufika bandani.
“Sina furaha, yoyote,” Sharifu akajibu.
“Mbona nakuona, unaimba na kucheza kwa furaha?.”
“Najiimbia tu mama yangu, nisichoshwe na kazi,” Sharifu alijibu huku akizoa kinyesi cha kuku na kukiweka kwenye ndoo ya taka.
“Umenikumbusha mbali.”
“Kivipi?.”
“Nyimbo hiyo unayoimba inanikumbusha miaka ya tisini na nne hivi, kipindi alichonioa baba yako alikuwa anapenda kweli kuimba nyimbo hiyo.”
“Kweli?.”
“Eehe!.”
“Nyimbo hii unajua, kanifundisha nani.”
“Sijajua.”
“Kanifundisha baba huyo huyo.”
“Nilijiuliza huyu mtoto nyimbo hii kaitoa wapi, kumbe umefundishwa na baba yako.”
“Eenh...natoka siku hiyo nimetokea kuipenda kweli hiyo nyimbo.”
“Ulikuwa kumbe na baba mzuri sana?.”
“Sana tena sana kwa jinsi alivyokuwa ananipenda baba hadi leo hii angekuwepo nisingetaabika,” Sharifu alijibu kisha akabeba ndoo na kwenda kumwaga kinyesi cha kuku.
Binti Mngane alipohakikisha mwanae amemaliza kufagia banda la kuku alikwenda ndani kukaa kwenye mkeka ukumbini. Sharifu alipomwaga taka akajongea hadi chumbani na alipofika kitandani akajitupa kifudifudi masaa mawili mbele. Sharifu akak**atwa na usingizi mzito, akiwa amesinzia akaingia Mzee Damanda chumbani kwake kimiujiza na kuanza kuzungumza naye kupitia ndoto.
“Kibaraka wangu,” Mzee Damanda akaita.
“Naam” aliitika Sharifu ndotoni.
“Nimekuja, kuna jambo limenileta.”
“Jambo gani?.”
“Umepita mwezi sijawaona kilingeni kulikoni?.”
“Kulikuwa kuna mambo kidogo tunaweka sawa.”
“Unakumbuka katiba yetu?.”
“Nakumbuka.”
“Zipi?.”
“Usimjaribu mwanachama mwenzio. Usitangaze siri za chama na kuhudhuria kilingeni kila siku.”
“Safi...mbona nyinyi mnakiuka katiba?.”
“Tunapitiwa kiongozi wetu...lakini kuanzia leo nakuahidi hatutokosa kilingeni.”
“Sawa...naondoka ila mkae mkijua nisipowaona siku zijazo nitajua cha kufanya.”
“Nimekuelewa kiongozi, kuanzia leo tutakuwa kilingeni pamoja wala hatutokuangusha tena.”
Mzee Damanda alipoondoka, Sharifu akakurupuka ndotoni. Akanyanyuka kitandani akaelekea moja kwa moja alipo mama yake. Akamkuta mama yake ukumbini ameketi kwenye mkeka na hawamu hii akiwa anamenya ndizi.
“Mama,” Sharifu akaita.
“Eeehe niambie...naona umeshaamka,” Binti Mngane aliongea huku macho yake yakitazama chini akichukua ndizi nyingine.
“Nimeamka...lakini nimeamka na habari mbaya” aliongea Sharifu kisha akasimama mbele ya mama yake sawa sawia.
“Kutoka, wapi?” aliuliza Binti Mngane kwa kutahamaki.
“Kwa, Mzee Damanda.”
“Anashida gani tena?.”
“Kaja kutupa onyo kwa sababu hatuhudhurii kwenye kilinge.”
“Mh! ni kweli...sasa wewe ulimwambiaje?.”
“Sikumwambia chochote, zaidi ya kukiri kosa na kuomba msamaha.”
“Nakuasa mwanangu tujirekebishe bila hivyo mwaka huu tutaumbuka.”
Sharifu baada ya kuzungumza na mama yake akamuaga mama yake kuwa anakwenda nyumbani kwa kina Kondo kupiga stori kidogo. Mama yake akamruhusu aende lakini wakati anaanza safari njiani akakutana na bibi kikongwe asiyeweza kutembea kutokana na kuvimba miguu.
“Mjukuu wangu” aliita Kikongwe yule mara baada ya kumuona na kupishana naye Sharifu.
“Naam” aliitika Sharifu kwa busara.
“Naomba msaada.”
“Msaada upi?.”
“Wa kunipeleka nyumbani.”
“Sitoweza bibi kuna mahali nawahi.”
“Naomba unipeleke nitakupa zawadi tukifika nyumbani kwangu,” Kikongwe yule alimrubuni Sharifu kwa zawadi.
“Zawadi ipi?.”
“Wewe nipeleke zawadi hiyo utaiona tukifika,” Sharifu akakubali kumpeleka Kikongwe yule kwake kwa kumbeba mgongoni kwa sababu ya kutoweza kutembea vizuri.
Wakiwa wapo njiani Sharifu akahisi maumivu makali mgongoni. Akapeleka nyuma mkono wake wa kuume kulipo na maumivu ili apate kuthibitisha k**a kweli ana jeraha au laa. Ghafla yule bibi akabadilika kuwa Chui mwenye miguu minne na kumrarua Sharifu mkono alioupeleka nyuma kupapasa.
Sharifu akamtupa pembeni kikongwe yule kwa hasira. Baada ya kutupwa kikongwe yule akawa anacheka kwa sauti ya juu huku sauti yake ikisikika kufika masafa ya mbali.
“Msaada ninaotaka kukupa unaona haufai? Unaamua kunidhuru?,” Sharifu aliongea kwa ghadhabu.
“Lengo langu si msaada kutoka kwako lengo langu ni kukuua,” Kikongwe yule alisema kwa ujasiri uliotukuka. Sharifu akacheka kisha akasema naye kwa ujasiri bila hofu.
“Unajiamini sana...ngoja nami uone nipoje.”
Sharifu muda huo huo naye akabadilika kuwa Simba mwenye pembe ndefu na meno makali mithili ya sindano.
Alipojibadilisha vile tu moja kwa moja akamvamia kikongwe yule aliyejibadili Chui na kupeana mikong'oto ya haja. Mikong'oto ikatembezwa yapata masaa mawili kisha kila mmoja akawa pumzi kisoda. Sharifu hakukubali kushindwa japo alichoka lakini akamkabili vyema kikongwe yule na hatimaye kikongwe yule akashindwa akatafuta upenyo akakimbia. Sharifu akacheka sana na akaongea kwa dharau.
“Ulijua nipo kijingajinga, nina nguvu balaa. Nenda kajipange na nguvu zako za mtoto mchanga.”
Sharifu akahairisha hadi safari yenyewe kutokana na kuchafuka mara baada ya kurudi kwenye hali ya ubinadamu akarudi nyumbani.
Akafika nyumbani akakuta kumetulia na hadi mama yake hakuwepo. Hakuwa na shaka sana, hivyo akaingia chumbani huku moyoni akijiuliza baadhi ya maswali.
“Kikongwe yule katokea kijiji gani?..na lengo la kuniua ni nini?.”
“Mama anaweza kumjua kweli?..looh! simjui hata jina kikongwe yule.”
“Nitamweleza mama kwa maumbile, k**a atamjua anitajie jina lake nimjue.”
Sharifu akiwa yupo kitandani bado akiwa anajisemesha mara usingizi ukamjia na akawa anakoroma bila kujijua. Masaa kadhaa mbele alikuja kushtuka mara baada ya kusikia mlango wake wa chumbani ukigongwa. Akakurupuka kutoka kitandani na kwenda kumfungulia anayegonga.
“Mama ulikuwa wapi?,” Sharifu aliuliza mara baada ya kuona kuwa aliyekuwa anagonga ni mama yake.
“Nilikuwa mtaa wa pili nikiazima p**a la kupikia pombe...si unajua kesho pombe kwangu?,” Binti Mngane akajibu na kuuliza.
“Umelipata p**a lenyewe?.”
“Nimelipata...ila ni chafu kanisaidie kuliosha.”
“Kuna kazi kwa sasa unataka kufanya?.”
“Nataka nifue nguo mara moja maana zimekuwa chafu sana.”
“Sawa...mimi ngoja nikasafishe p**a hilo,” Sharifu baada ya kupeana majukumu na mama yake, kila mmoja akaingia katika kazi yake.
Baada ya saa moja wote wakawa wamemaliza kazi wakaenda kuketi ukumbini kwa pamoja wapige soga. Sharifu akaanzisha mazungumzo mara baada ya ukimya wa mama yake wa muda mrefu.
“Mama, hivi hapa kijijini kwetu kuna bibi vikongwe wangapi?.”
“Wawili,” Binti Mngane alijibu huku akitabasamu.
“Nani na nani?.”
“Bi Kazimoto na Bi Tuni...kuna nini kwani?.”
“Leo njiani, nimekutana na bibi kikongwe akanidhuru.”
“Yupoje, kikongwe huyo?.”
“Miguu yake, imevimba na mfupi.”
“Oooh!, huyo atakuwa Bi Kazimoto.”
“Unamjua?.”
“Eeenh!.”
“Anaishi wapi?.”
“Ni jirani yetu, anaishi nyumba tatu za mbele zinazofuata...alitaka kukudhuru kisa nini?.”
“Sijajua...sio kunidhuru tu, alitaka aniue kabisa.”
“Toba!!!, majirani wananitafuta nini?..ujaumia sana?.”
“Sijaumia sana ameniweka kajeraha kidogo tu...lakini nina hasira naye.”
“Unatakaje?.”
“Kama unapajua kwake, baadaye unipeleke nik**alize hasira zangu.”
“Usijali, baadaye tukitoka kilingeni nitakupeleka,” Binti Mngane alipiga soga na mwanae hadi nyakati za kupika chakula zikafika.
Akanyanyuka kwenye mkeka pale ukumbini na kuelekea jikoni kupika chakula cha usiku. Sharifu hakutaka kuendelea tena kukaa pale ukumbini. Akaamua kuchukua mkeka na kwenda kujilaza nje kwaajili ya kupunga upepo wa jioni.
**********
Nyumbani kwa Bi Kazimoto furaha haikuwepo. Alikuwa anawaza na kuwazua kwa jinsi alivyokosa ushindi.
“Mtoto yule anatumia uchawi wa aina gani?..atakuwa anatumia uchawi wa kale nini?.”
“Yaani kitoto kile kinishinde mimi............? Sikubali nitajipanga tena.”
Bi Kazimoto kwa siku ile ilikuwa ya huzuni kwake na mbaya zaidi kila akifikiria tukio lile. Akahisi homa, yaani hakutamani hata chakula cha aina yoyote kipite kinywani mwake. Yaani siku ile chakula hakikuwa kitamu upande wake hivyo akalala bila kula kitu chochote siku hiyo.
**********
Binti Mngane alipoivisha chakula na kula yeye na mwanae wakaingia kila mmoja kwenye chumba chake kwa ajili ya kwenda kujipumzisha mwili. Binti Mngane akiwa usingizini akazama moja kwa moja kwenye ndoto, ndoto ikampeleka ajione yupo na mumewe wanazungumza.
“Mwanamke mbaya sana, yaani umeniua kwa kunitoa kafara kwasababu ya kunufaisha uchawi wako,” Baba Sharifu alinung'unika kwa kumnung'unikia mkewe kwa kumwaisha kaburini.
“Si kusudi langu, ni kusudi la mizimu kunilazimisha kutoa kafara kinguvu,” Binti Mngane alijitetea ili asionekane mbaya na mumewe.
“Mbona hujamweleza mtoto uchafu uliofanya...halafu unajitetea leo. Lazima nikuue,” Baba Sharifu aliongea na kutaka kupeleka mikono yake kwenye shingo ya mkewe amkabe.
“Tobaaa!!!, roho yangu,” Binti Mngane alishtuka kwa kukurupuka ndotoni huku akihema kwa kasi k**a mwizi aliyekimbizwa na raia.
Sharifu kwa makelele ya mama yake akashtuka usingizini. Akaamka na kwenda chumbani kwa mama yake akaone kilichomkuta mama yake.
SASA TUNAENDELEA KUCHUKUA ODA KWA KITABU HIKI 👇. BADO WATU 47 TU IWE MWISHO WA KUCHUKUA ODA....WEKA ODA LEO IWE RAHISI KUKIPATA HIKI KITABU KWA BEI YA TSHS. 10000/= TU... 🙏.