25/09/2020
SHIDA YA KUOA USTADHAT
Ustadh alitaka kuongeza *Mke* wa pili akataka kuchukua rai kutoka kwa Mkewe kwa njia ya hikma:
*MUME:* Wajua Sayyidna Ali bin Abitalib alioa wake wangapi?
*MKE* Alioa Wake wengi kwaiyo na wewe unataka kusema nini??
*MME* Nataka kuishi Maisha ya kisunna k**a Alivyoishi Saydina Ali.
*MKE:* (Ashashtuka hapo) Wewe wajua Sayyidna Ali alipigana vita vya jihadi vingapi? K**a wataka kuwa k**a yeye si ungekwenda ukaikomboa Masjid Aqswa kutoka kwa mayahudi!
*MUME:* (Alikuwa Kasimama Akakaa Kwanza..)
*MKE:* Katika vita vya Bani Khaybar, Sayyidna Ali alikwenda akavunja mlango wa ngome ya mayahudi na kuwashinda. Wewe juzi mwanao amejifungia chooni tu mlango umekushinda mpaka tukaleta fundi!
*MUME*(Alikuwa kakaa akavua viatu, na kofia akaweka mezani..)
*MKE:* Sayyidna Ali alikua akifanya ibada usiku jangwani peke yake mpaka akipotewa na fahamu kwa khushuu. Wewe ukiona panya tu hapa waweweseka mpaka usingizini.
*MUME* (Akavua kanzu akajitupa kitandani.)
*MKE* Wakati wa Hijra Sayyidina Ali aliachiwa mali za Watu na Akawarudishia wenyewe Zote bila kupunguza
Wewe umeachiwa Mali za urithi una Kazi ya kugombana na ndugu zako tu kila siku kuwagawia hutaki
Halafu wataka uwe km Sayidna Ali labda uwe Ali Kiba.
*MUME:* Basi Mke wangu yaishe hebu mlaani sheitwani tulale sasa.
ZAUJ WA Zaujaty