08/06/2016
*******Je Computer yako iko slow sana kupita kawaida??*********
Mambo 10 yanayofanya computer kuwa slow ni k**a ifuatavyo.
1. Program zaidi ya 3 zinafanya kazi kwa wakati mmoja.
JIBU: funga program zote ambazo hauzitumii kwa muda huo na ubakize tu ile unayotumia kwa wakati huo.
2. Computer haina RAM yakutosha
JIBU: Nenda kwa wataalamu wa computer ununue RAM inayoingia kwenye computer yako uongeze RAM itasaidia
3. Computer yako inaweza kuwa na Virus.
JIBU: Njia pekee yakuondoa Virus kabisa kwenye computer ni kufuta kila kitu na kuweka upya Operating system. lakini unaweza pia kufanya scanning na ikasadia kwa sehemu.
4. Hard disk ya computer yako imejaa.
JIBU: Toa vitu visivyo na umuhimu kwenye computer hususan katika disk yenye operating system, inashauriwa kuwa na angalau GB 30 free.
5. Ni muda umepita tangu uzime computer yako.
JIBU: Unapozima computer inapata muda wa kupumzika na kuanza kazi vizuri ni k**a mtu anavyokwenda kulala.
6. Ni muda mrefu umepita huja update computer yako.
JIBU: Fanya update ya computer yako na antivirus uliyoweka.
7. Umeweka mbwembwe(effects) nyingi kwenye screen yako i.e saa, slideshow ya picha zako N.K.
JIBU: Punguza madoido kwenye screen ya computer yako na ondoa program zote zisizo na faida yoyote kwako.
8. Kuna Program inafanya kazi chini kwa chini bila wewe kujua. Mfano: Antivurus.
JIBU: Hakikisha hakuna program yoyote inayofanya kazi chini kwa chini bila wewe kujua. (Bonyeza SHIFT+CTRL+ESC) ili kuona program zinazo fanya kazi.
9. Computer yako inaweza kuwa haina uwezo wa kutumia software ulizoweka.
JIBU: kabla hujaweka program yoyote kwenye computer yako hakikisha kuwa computer yako ina uwezo wakubeba ile program.
10 Hard disk yako imekaribia kufa, au kufikia mwisho wa matumizi yake.
JIBU: Badili hard disk ya computer yako.
Natumaini maelezo haya yatakusaidia katika utumiaji wa computer yako.
K**a una maswali zaidi au unahitaji msaada wa kiufundi zaidi wasiliana nasi kwa:
[email protected]
+255 785 012 531
+255 717 645 446
P.O.Box 14741
Arusha
Tanzania
Au fika ofisni kwetu ARUSHA, NJIRO Mtaa wa Tanesko kwenye Geti la TANALEC