KANDA YA ZIWA KWETU

KANDA YA ZIWA KWETU Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from KANDA YA ZIWA KWETU, Mwanza.

26/09/2021

UNATOA MAONI GANI HAPO KWA NDOA YA AINA HII?

SALAAM ZA RAMBIRAMBI:-------------------------------------------Nimepokea taarifa ya musiba wa Raisi wa Jamuhuri ya Muun...
18/03/2021

SALAAM ZA RAMBIRAMBI:
-------------------------------------------

Nimepokea taarifa ya musiba wa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshiwa Dr. John Joseph Pombe Magufuli kwa majonzi makubwa.

Natoa salaam za rambirambi na pole kwa huu musiba mkubwa uliolikumba taifa letu, kuondokewa na Raisi wetu mpendwa, hodari, imara na mchapa kazi.

Najua jambo hili limegusa moyo wa kila mmoja. Niwatie Nguvu, bado Mungu yuko upande wa taifa letu ataendelea kuwa mfariji, kiongozi na mlinzi mkuu kwa taifa letu.

Aidha, tuwaombee sana viongozi wetu wa Serikali, hasa Mh. Makamu wa Raisi, Mama Samia Suluhu Hassan na baraza la mawaziri, Mungu awe pamoja nao katika wakati huu. Mungu awapatie uvumilivu, hekima na ujasiri wa kisimamia mambo yote katika uzoefu ngumu na mpya wanayopitia.

Tuiombee sana familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki. Mungu awe faraja kwao, yeye pekee ndiye atakayeziba pengo hili.

Hata hivyo, sisi wananchi, Mungu aliotujalia nuru, tuoneneshe Ukomavu katika Imani, na kuwatia watu wa Mungu moyo.

Ni vema pia kuwa makini katika usemi wetu. Tuombe Mungu atakase vinywa vyetu, maneno yetu yawe ya Neema siku Zote, tujue la kumjibu kila Mtu......( Kolosai 4:6).

Tushirikiane ombi hili la Daudi;
" Utufundishe ufupi wa maisha yetu ili tuweze kuwa na hekima" ( Zaburi 90:12 - Kiswahili cha Kisasa).

Wapendwa, tuwajibike kuliko kawaida kwani muda ni mchache. Mtumishi wa Mungu Daudi alilijua hilo.

Nawatakia faraja kutoka kwa Mungu. (2 Kor. 1:3,4).

______________________________________________________________

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

10/02/2021

MKURUGENZI wa Taasisi ya Utafi ti ya Dawa Asili Muhimbili (MUHAS), Dk Joseph Otieno, amesema kujifukiza ni tiba ambayo ikitumika vizuri, inaboresha mfumo wa upumuaji na kuusaidia mwili kupata nguvu ya kupambana na maradhi.

Dk Otieno alisema kwenye mlipuko wa virusi vya corona, ni vyema wananchi bila kujali k**a wameathirika au la, wajenge tabia ya kujifukiza angalau mara mbili kwa siku ili kuukinga mwili usipate virusi hivyo. Kwa mujibu wa Dk Otieno, kujifukiza ni tiba iliyokuwa ikitumika katika jamii nchini na ilionesha matokeo chanya.

“Nasisitiza tena k**a nilivyosisitiza mwaka jana wakati wa janga la corona lilipoingia nchini, kujifukiza kwa njia sahihi ni kinga dhidi ya maradhi haya, cha msingi ni kutumia viungo sahihi na kufuata maelekezo jinsi ya kuvichanganya na kujifukiza,”alisema.

Alizungumzia namna ya kudhibiti virusi vya corona kwa kutumia njia za asili ikiwemo ya kujifukiza maarufu kupiga nyungu, Dk Otieno alishauri kuwa kwa mazingira ya Tanzania, aina tatu za majani zinapatikana kwa urahisi na zimefanyiwa utafiti na kuthibitika ubora wake, lakini pia zina machapisho.

Alitaja majani hayo kuwa ni ya kivumbasi (kashwagala), mkaratusi na mchaichai. Alisema usalama wa majani hayo, umethibitika na yana mafuta tete yanayosaidia kufungua mfumo wa upumuaji ili mwili upate nguvu ya kupambana na maradhi.

“Nyungu inafaa sana k**a virusi bado viko kwenye mfumo wa upumuaji havijaingia kwenye seli za damu, kwa sababu unapojifukiza kwa kutumia vitu hivyo vitatu kwa njia sahihi, hayo mafuta tete yanapenya vizuri na kuingia kwenye mfumo wa upumuaji na kuuzibua, hapo mwili unapata nguvu na kupambana vizuri’’alisema Dk Otieno.

Alisema, iwapo virusi vya corona vitakuwa vimeingia kwenye seli za damu, njia sahihi ya kuusaidia mwili kupambana navyo ni kutumia maji ya moto yaliyochanganywa na tangawizi ili kusaidia damu isigande kwenye mishipa wakati huo mwili ukipambana na virusi.

Dk Otieno alisema kiungo kingine kinachofanya kazi sawa na tangawizi katika kupambana na corona ni kitunguu saumu, ambacho kazi yake ni kusaidia damu isigande wakati mwili unapambana na maradhi.

Alisema kitunguu saumu katika tiba hii, kinatakiwa kisagwe na kuwekwa kwenye maji baridi au kukitafuna kibichi, kwa sababu ukikichemsha unaua nguvu yake na hapo hakitafanya kazi kusudiwa.

Kwa mujibu wa Dk Otieno, kwa kawaida virusi havina tiba na vinapoingia mwilini hupambana na kinga ya mwili na k**a mwili ukiwa na kinga nzuri huvishinda na kuviua, lakini ukiwa na kinga dhaifu mwili hushindwa kupambana navyo na matokeo yake ni kifo. Alisema watu wengi hukosea namna ya kujifukiza, kwa kuwa wanachemsha majani ya mimea hiyo hadi yanapoteza mafuta tete yanayohitajika.

Dk Otieno alisema ili kujifukiza, inabidi kuchemsha maji hadi yatokote kisha unaweka majani ya mchaichai, mkaratusi na kivumbasi (kashwagala) na kukoroga, kisha kuyaepua na kuanza kujifukizwa kwa kujifunika na shuka zito au blanketi kwa dakika kati ya tano hadi 10 kulingana na uwezo wa mwili.

“Wengi wanakosea wanadhani unachemshia hivyo vitu huko wee, kufanya hivyo unaua mafuta tete yote yanayohitajika,”alisema.
Dk Otieno alisema kujifukiza si lazima mtumiaji atumie vitu hivyo vitatu, anaweza kutumia kimojawapo na kuzingatia maelekezo, afanye hivyo kwa mara mbili kwa siku na kusisitiza kujifukiza kuwa sehemu ya maisha ya wananchi kila siku.

Alisema mtu anayejifukiza anapaswa kufunga macho, kuachama mdomo na pua, kisha aendelee kuhema kawaida ili kuruhusu mvuke kupita kwenye mfumo wa upumuaji na akishaepua nyungu, akoroge mara moja ili ule mvuke mkali utoke kisha ndio ajifunike na shuka au blanketi.

Alishauri kuwa wagonjwa, wazee na watoto, wasijifukize ila wanywe maji ya moto yenye tangawizi, au iliki na mdalasini.

Address

Mwanza

Opening Hours

Monday 00:00 - 12:00
Tuesday 00:00 - 12:00
Wednesday 00:00 - 12:00
Thursday 00:00 - 12:00
Friday 00:00 - 12:00
Saturday 00:00 - 12:00
Sunday 00:00 - 12:00

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when KANDA YA ZIWA KWETU posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share