08/01/2020
Binti alikuwa mfanya kazi wa kazi za ndani siku moja asubuhi alipokea simu kutoka kwa mwajiri wake.
Boss alisema: naomba leo usije kazini nimeshaweka mtu mwingine kwenye nafasi yako.
Binti alilia sana maana familia yake ilikuwa inamtegemea na huo mshahara ndo ulikuwa chanzo pekee cha kujipatia riziki.
Wakati analia alisikia sauti za watu waliokuwa wakipita njia huku wakitiana moyo, mtu mmoja alisikika akisema:-
Mshukuru Mungu kwa kila jambo, Mungu hawezi akakuacha hivi hivi, shida, taabu na matatizo ni mitihani ayokupa hivyo kadili unavyoipita ndiyo unasogea kwenye baraka zake, leo umekosa huenda kesho ndo zamu yako usikate tamaa.
Binti ajipa matumaini, alichukua bibilia akapiga magoti akaanza kusali. Alifanya maombi asubuni na jioni, aliomba kila akitaka kulala na kila akiamka huku akiendelea kutafuta kazi.
Siku moja moja wakati yupo mtaani akizurula kutafuta kazi alikutana na kijana, kijana akamwambia:- samahani, unaweza kuja ukanisaidia kufanya kazi ofisini kwangu?
Mfanyakazi wangu hajaja nasikia amehama na hajanipa taarifa yoyote.
Binti akasema: lakini mimi nilikuwa nafanya kazi za ndani na sijui chochote mambo ya ofisi staff.
Kijana akamwabia: usiwe na hofu nitakufundisha kila kitu.
Binti alienda kumsaidia huyo kijana na kijana alifurahishwa na utendaji wa kazi wa huyo binti akamwajiri na kuwa anamlipa mshahara mkubwa mara 10 zaidi ya ule aliokuwa akilipwa huko alikotoka na mwisho akamtafutia nafasi shuleni akaanza kumsomesha.
Binti alipiga magoti na kusema:- hakika wewe Mungu ni mwema umejibu maombi yangu, asante Mungu.
Riziki ya mwanadamu ipo kwa mwenyezi Mungu
Mungu wabariki wote watakao shiriki au kuisambaza post hii "amen"
to see the future post
By Joseph Lawrence Jigalu