13/02/2025
Umeitazama SNOWFALL?
Nimeanza kuifuatilia hii series ya Snowfall, ni moja ya series kali sana lakini unatakiwa usiwe na presha unapoanza kuiangalia, na imenifundisha baadhi ya mambo.
1. Unatakiwa kujua unataka nini, huwezi kukurupuka kufanya biashara huku ukiwa hujui unataka nini.
2. Unapoanza kufanya biashara na mtu fulani, hata k**a yeye anakuuzia bidhaa, jitahidi sana na wewe utengeneze bidhaa zako, yaani k**a kutafuta mzigo sehemu nyingine, usitake kuchukua mzigo sehemu moja.
3. Unapoanza kutengeneza njia ambayo unaamini ina mafanikio, usimsikilize mtu mwingine, hata k**a ni mama yako atakwambia hiyo njia si sahihi, k**a unaamini ni sahihi, nenda nayo. Utakapohustle, utahustle peke yako tu.
4. Chagua kampani ya kufanya nayo kazi pamoja, usichukue rafiki ambaye unaona kabisa hawezi kusapoti hiki ninachokifanya. Ukiona rafiki hasapoti, mteme, katafute wengine unaoona nitapambana nao bega kwa bega.
5. Hutakiwi kuwa na huruma hata kidogo. Biashara ili isimame unatakiwa kuwa na roho mbaya.
6. Usiwe mtu wa kupaniki kwenye kufanya maamuzi, calm down, think halafu fanya jambo. Kamwe usifanye maamuziki ukiwa na hasira.
7. Jua ukifeli, umefeli maisha yako na si ya mtu mwingine.
8. Mshirikishe mpenzi wako ajue biashara unayoifanya, mwisho achague kuendelea kubaki na wewe ama ale njia yake.
9. Hata uwe bize vipi, hata uwe unapambana na kukosa muda, jitahidi sana uwe unafanya mapenzi kuirefresh akili yako.
10. Mtu akimess up na biashara yako, mess up na maisha yake.