Ema rich

Ema rich Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Ema rich, Shopping & retail, Kiungani na congo, Dar es Salaam.

11/05/2026
18/12/2024

■ CHRISTMAS SIYO X-MAS!

■ K**A WEWE NI MKRISTO, MAJIRA HAYA YA CHRISTMAS, USINASWE KATIKA MTEGO WA IBILISI, WA KUANDIKA, AU WA KUSEMA, "X-MAS", BADALA YA "CHRISTMAS"

"Kwa hiyo NITAKUWA TAYARI KUWAKUMBUSHA HAYO SIKUZOTE, IJAPOKUWA MNAYAJUA na kuthibitishwa katika Kweli mliyo nayo. Nami naona ni haki, maadamu nipo mimi katika maskani hii, kuwaamsha kwa kuwakumbusha" (2 PETRO 1:12-13).

K**a wewe ni Mkristo, majira haya ya Christmas, usinaswe katika mtego wa Ibilisi (2 TIMOTHEO 2:26); wa kuandika, au wa kusema, "Xmas"; badala ya "Christmas".

Inatupasa kukumbuka kwamba, Yesu anaitwa pia, Kristo (MATHAYO 1:16; 27:22). Na tena, inatupasa kufahamu jinsi mojawapo ya kupambanua kati ya Roho wa Mungu, na roho ya Ibilisi; au ya Mpinga Kristo. Kila roho inayokiri kwamba Yesu Kristo amekwisha kuja katika mwili, hapa duniani; yatokana na Mungu, na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu; bali hiyo ndiyo roho ya Mpinga Kristo, ambayo imekwisha kuwako duniani. Neno la Mungu katika 1 YOHANA 4:2-3, linasema, "Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. NA HII NDIYO ROHO YA MPINGA KRISTO ambayo mmesikia kwamba yaja; NA SASA IMEKWISHA KUWAKO DUNIANI."

Roho hii ya Ibilisi, ya Mpinga Kristo; ilidhihirika tangu nyakati za Mafarisayo, wakati wa huduma ya Yesu Kristo; alipokuwapo duniani. MAFARISAYO, HAWAKUWA TAYARI kutaja Jina la YESU, au la KRISTO; bali waliyakwepa majina hayo yote, na WALIMWITA Yesu Kristo, "YULE". Mafarisayo hawa, walikuwa wepesi kutaja jina la Musa, lakini hawakuwa tayari kulitaja Jina la Yesu. Waliona kwamba, kutaja Jina la YESU, ilikuwa ni KUKIRI kwamba, Yesu Ndiye MWOKOZI wa Ulimwengu; atakayewaokoa na dhambi zao (MATHAYO 1:21; 1 YOHANA 4:14; YOHANA 4:42); wakati wao hawakuwa wakimwamini; kwa sababu hiyo, hawakuwa tayari kufanya hivyo. Waliona pia, kwamba, kutaja Jina la KRISTO, ilikuwa ni KUKIRI kwamba, Yesu Ndiye Masihi; kwa kuwa neno Kristo, maana yake ni Masihi; wakati wao hawakuamini kwamba Yesu, Ndiye Masihi aliyetabiriwa; Aliyekuja duniani (YOHANA 4:25-26). Hivyo, wakaamua kumwita, "YULE". Tusome sasa, YOHANA 9:28, "Basi wakamshutumu, wakasema, Wewe u mwanafunzi wake YULE; sisi tu wanafunzi wa MUSA."

Siyo hilo tu, bali pia, Nyakati za Mitume wa Kanisa la Kwanza; roho hiihii, ndiyo iliyowafanya Mitume kupigwa na kuamuriwa WASISEME au WASINENE kwa JINA LA YESU! Tunasoma katika MATENDO YA MITUME 4:18, "Wakawaita, WAKAWAAMURU WASISEME KABISA wala kufundisha KWA JINA LA YESU." Tena tunasoma katika MATENDO YA MITUME 5:40, "Wakakubali maneno yake, nao walipowaita Mitume, WAKAWAPIGA, WAKAWAAMURU WASINENE KWA JINA LAKE YESU; kisha wakawaacha waende zao." Je, Mitume walikubali kuacha kulitaja Jina la Yesu Kristo? JIBU NI LA! Waliendelea kulitaja na kuhubiri kwamba Yesu Ndiye Kristo (MATENDO YA MITUME 4:18-20; 5:40-42).

Unaweza kuona! Kumbe basi, inatupasa kufahamu kwamba, roho ileile ya Ibilisi na ya Mpinga Kristo, iliyowafanya Mafarisayo kumwita Kristo, "YULE" nyakati zile; ndiyo inayotaka na sisi tumwite Kristo, "X"; nyakati hizi za leo; na hivyo, badala ya kuandika "CHRISTMAS", eti tuandike "X-MAS". Mitume hawakukubali, NA WEWE USIKUBALI, kuacha kuandika Jina hilo la CHRIST yaani KRISTO; ambalo Ndilo Jina Kuu kuliko majina YOTE (WAFILIPI 2:9-11); na wala usisikilize maneno yao ya kutunga kwa werevu, ya kuhalalisha kufanya hivyo (2 PETRO 2:1-3). Usilionee haya KAMWE, Jina la Yesu Kristo! (MARKO 8:38). Mwenye masikio, na asikie! (MATHAYO 11:15).

Hbd my mamy ake mama Ako nakupenda sana sana NA NAMWOMBA MUNGU akupe miaka mingi ya kuishi na maisha mema yenye kumpende...
15/01/2024

Hbd my mamy ake mama Ako nakupenda sana sana NA NAMWOMBA MUNGU akupe miaka mingi ya kuishi na maisha mema yenye kumpendeza yeye

13/01/2024
03/06/2023

Karibuni tutengeneze majiko yetu yawe mwaaaa

Address

Kiungani Na Congo
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ema rich posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share