NOOR International kiswahili

NOOR International kiswahili Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from NOOR International kiswahili, Book shop, السعودية, Riyadh.

Wale watoao mali zao usiku na mchana, kwa siri na kwa dhahiri, basi wana malipo yao kwa Mola wao, na hawatakuwa na hofu ...
16/07/2026

Wale watoao mali zao usiku na mchana, kwa siri na kwa dhahiri, basi wana malipo yao kwa Mola wao, na hawatakuwa na hofu yoyote na hawatahuzunika (AL-BAQARAH: 274)

Baadhi ya nyoyo hutoa vipawa vyao kwa siri, hazisubiri kusifiwa wala hazitafuti kuonwa na watu.

Zinatambua kuwa Allah anaziona, na hilo tu linawatosha.

MAZINGATIO:
Sadaka na kutoa kwa siri ni nuru ya Qur’an.

Enyi ambao mmeamini wasicheze shere watu miongoni mwa watu huenda wakawa bora kuliko wao, wala wanawake kwa wanawake hue...
15/07/2026

Enyi ambao mmeamini wasicheze shere watu miongoni mwa watu huenda wakawa bora kuliko wao, wala wanawake kwa wanawake huenda wakawa bora kuliko wao wala msizidharau nafsi zenu wala msipeane majina mabaya ya uovu baada ya imani, na yeyote asiye tubu basi hao ndio madhalimu (AL-HUJURAAT : 11)

’ani_Tukufu

14/07/2026

Na (makafiri) wakitaka kukuhadaa (kwenye suluhu na amani) basi Allah anakutosha (dhidi ya hila na khiyana zao). Yeye (Allah) ndiye aliyekupa nguvu kwa nusra yake na kwa waumini

Na ameziunganisha nyoyo zao[1]. Lau k**a ungetoa vyote vilivyomo duniani usingeweza kuziunganisha nyoyo zao, lakini Allah ndiye aliyewaunganisha[2]. Hakika, Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye hikima (AN-FAL : 62-63)

Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allah ni k**a mfano wa punje iliyotoa mashuke saba, ikawa katika kila shu...
13/07/2026

Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allah ni k**a mfano wa punje iliyotoa mashuke saba, ikawa katika kila shuke mna punje mia. Na Allah humuongezea amtakaye, Na Allah ni Mwingi wa fadhila, Mjuzi mno (AL-BAQARAH : 261)

Uzuri ulioje katika kutoa!
Hakika unapotoa huwezi kuona matunda yake yote, lakini Allah anayaona, na hujaalia kutoka katika vichache na kuwa kheri nyingi zenye kuongezeka maradufu.

MAZINGATIO:
Ukarimu na kujitolea katika kheri ni nuru ya Qur’an.

Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allah ni k**a mfano wa punje iliyotoa mashuke saba, ikawa katika kila shu...
12/07/2026

Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allah ni k**a mfano wa punje iliyotoa mashuke saba, ikawa katika kila shuke mna punje mia. Na Allah humuongezea amtakaye, Na Allah ni Mwingi wa fadhila, Mjuzi mno (AL-BAQARAH : 261)

Kutoa sadaka katika mizani ya kidunia huonekana ni kupungukiwa.

Lakini katika mizani ya Allah ni chanzo kikubwa cha wingi wa mafanikio.

Mtu anapotoa punje ndogo tu, basi huenda ikazalisha mashamba mengi ya kheri bila kutegemea.

MAZINGATIO:
Sadaka na kutoa katika kheri ni nuru ya Qur’an.

Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allah ni k**a mfano wa punje iliyotoa mashuke saba, ikawa katika kila shu...
11/07/2026

Mfano wa wale wanaotoa mali zao katika njia ya Allah ni k**a mfano wa punje iliyotoa mashuke saba, ikawa katika kila shuke mna punje mia. Na Allah humuongezea amtakaye, Na Allah ni Mwingi wa fadhila, Mjuzi mno (AL-BAQARAH : 261)

’ani_Tukufu

Wale watoao mali zao usiku na mchana, kwa siri na kwa dhahiri, basi wana malipo yao kwa Mola wao, na hawatakuwa na hofu ...
10/07/2026

Wale watoao mali zao usiku na mchana, kwa siri na kwa dhahiri, basi wana malipo yao kwa Mola wao, na hawatakuwa na hofu yoyote na hawatahuzunika (AL-BAQARAH: 274)

’ani_Tukufu

Basi ni kwa rehema za Allah umekuwa mpole kwao, na lau ungekuwa muovu wa tabia, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeku...
08/07/2026

Basi ni kwa rehema za Allah umekuwa mpole kwao, na lau ungekuwa muovu wa tabia, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangekukimbia, basi samehe na uwaombee msamaha na watake ushauri katika jambo, na ukitia azma ya jambo basi mtegemee Allah, hakika Allah anawapenda wenye kumtegemea (AL-IMRAN : 159)

Kiongozi bora huwa hawatukani watu, bali huwa na tabia ya kusamehe, na kusikiliza na kushauriana katika mambo.
Nyoyo hujengwa kwa tabia hizo njema, kabla ya kujenga maazimio yoyote.

MAZINGATIO:
Uongozi bora na tabia njema ni nuru ya Qur’an.

Basi ni kwa rehema za Allah umekuwa mpole kwao, na lau ungekuwa muovu wa tabia, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangeku...
07/07/2026

Basi ni kwa rehema za Allah umekuwa mpole kwao, na lau ungekuwa muovu wa tabia, mwenye moyo mgumu, bila ya shaka wangekukimbia, basi samehe na uwaombee msamaha na watake ushauri katika jambo, na ukitia azma ya jambo basi mtegemee Allah, hakika Allah anawapenda wenye kumtegemea (AL-IMRAN : 159)

Nguvu za kweli hazipatikani katika ususuavu (ugumu) wa moyo.

Bali zipo kwenye moyo unaojua namna ya kulainika.

Siku zote watu huupenda na kuukaribia moyo wenye huruma, na hujitenga na moyo mgumu usio na huruma.

MAZINGATIO:
Huruma na tabia njema ni nuru ya Qur’an.

Address

السعودية
Riyadh

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when NOOR International kiswahili posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category